Wanjiru Kihoro

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wanjiru Kihoro (1953 - 12 Oktoba 2006) alikuwa mwandishi na mwanaharakati wa kike kutoka nchini Kenya. Alikuwa kati ya waanzilishaji wa chama cha Akina Mama wa Afrika (AMwA) na Kamati kwa uhuru wa wafungwa wa kisiasa wa Kenya iliyopinga kufungwa kwa Wakenya wakati wa serikali ya Daniel arap Moi[1][2]

Elimu na kazi[hariri | hariri chanzo]

Alizaliwa Nyeri, Kenya akamaliza elimu ya shule ya upili kwenye Kenya High School huko Nairobi. Kihoro alisoma uchumi kwenye Columbia University, New York. Akachukua shahada ya pili ya Development Studies na shahada ya uzamivu kwenye Chuo kikuu cha Leeds (Uingereza) wakati wa miaka ya 1980.[1][2]

Alifunga ndoa na Wanyiri Kihoro wakawa na watoto wanne Wangui, Pambana, Amandla and Wairimu.

Mnamo 1982 Kihoro na mumewe walihamia London wakati serikali ya Arap Moi ilizidi kukamata na kufunga wapinzani nchini. Hapa alishiriki kuanzisha Kamati kwa uhuru wa wafungwa wa kisiasa wa Kenya. Alifanya kazi na The Africa Centre, London mwaka 1984 na baadaye na All African Conference of Churches na National Christian Council of Kenya na United Church Board for World Ministries.[1][2]

Mwaka 1985 alishiriki kuunda Akina Mama wa Afrika, na mwaka 1992 taasisi ya ABANTU for Development inayolenga kufundisha wanawake wa Kiafrika kwa nafasi za uongozi.[3]

Mwaka 2002 baada ya uchaguzi wa Mwai Kibaki alirudi Kenya.[1][2]

Kifo[hariri | hariri chanzo]

Mwaka 2002alipata ajali ya ndege na kupoteza fahamu kwa muda wa miaka minne na baadaye aliaga dunia mwaka 2006. [4]

Baada ya kifo chake gazeti la The Guardian likaandika ya kwamba "Wanawake wachache wa afrika wamejulikana vema kama Wanjiru Kihoro".[1] Wangui wa Goro aliandika: "alikuwa kiongozi, mwanaharakati kwa demokrasia, uhuru, haki za binadamu, usawa na haki akawa daima kwa upande wa wakereketwa hasa wanawake na maskini. Alichapa kazi bila kuchoka na kwa ujasiri."[5]

marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. 1.0 1.1 1.2 1.3 1.4 Haward, Patricia. "Wanjiru Kihoro", 22 November 2006. Retrieved on 23 August 2014. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 "Wanjiru Kihoro: an activist, feminist, patriot, visionary, leader, friend". Pambazuka News www.pambazuka.org. 19 October 2006. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-26. Iliwekwa mnamo 23 August 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)
  3. "Partner in Focus". Women's Environment and Development Organization www.wedo.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-09-20. Iliwekwa mnamo 15 September 2014.  Check date values in: |accessdate= (help)
  4. Telewa, Muliro. "Meeting 'Kenya's Terri Schiavo'", 6 April 2005. Retrieved on 23 August 2014. 
  5. wa Goro, Wangui (19 October 2006). "Wanjiru Kihoro: Sister, Comrade, Friend". Pambazuka News www.pambazuka.org. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2014-08-26. Iliwekwa mnamo 24 August 2014.  Check date values in: |date=, |accessdate= (help)

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]