Walther Bothe
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Walther Wilhelm Georg Bothe (8 Januari, 1891 – 8 Februari, 1957) alikuwa mwanafizikia kutoka nchi ya Ujerumani. Hasa anajulikana kwa kuvumbua njia mpya ya kutambua vijipande vya atomu. Mwaka wa 1954, pamoja na Max Born alikuwa mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fizikia.

