Wakerewe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kisiwa cha Ukerewe wanakotoka Wakerewe

Wakerewe ("abhakerebhe") ni kabila la watu wa kaskazini mwa Tanzania wanaoishi kwenye kisiwa cha Ukerewe katika Ziwa Viktoria. Lugha yao ni Kikerewe.

Kabila hili linaundwa na koo mbalimbali wakiwemo Abhanange, Abhasilanga, Abhakanda, Abhabhogo, Abhananila n.k.

Inaaminika kuwa kabila la Wakerewe lilitokea maeneo ya Bukoba, kisiwani Kerebe na walikuwa koo mbalimbali, hasa wakiongozwa na ukoo wa Abhasilanga ambao ndio wengi katika kabila hili. Mpaka leo kuna mawasiliano ya mbali kilahaja kati ya Wakerewe na kabila la Wahaya.

Kabila la Wakerewe lilikuwa likitawaliwa na kiongozi wao aliyeitwa Omukama, chini yake akifuatiwa na Omukungu ambaye alikuwa anatawala eneo dogo katika utawala wa Omukama, na wengine wakifuatia chini kama vile Katikilo n.k.

Mtawala wa Ukerewe alikuwa akimiliki kuanzia Ukerewe mpaka maeneo ya Mwibara ya Kisorya pia mpaka Irugwa Kisiwani.

Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wakerewe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.