Wahehe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wahehe ni kabila la Tanzania ambalo kiasili linaishi katika wilaya za kaskazini za Mkoa wa Iringa, yaani Iringa, Kilolo na Mafinga.

Ni moja kati ya makabila yaliyotokea kwenye bonde la mto Rufiji. Ndiyo sababu wanazika wafu wao wakielekea mashariki.

Lugha yao (Kihehe) imegawanyika kiasi fulani katika lahaja (matamshi) tofautitofauti kutokana na maeneo ambayo huzungumzwa. Inafanana kimatamshi na kimaana na lugha ya Kibena iliyopo wilayani Njombe.

Pamoja na Wabena wanahesabika kuwa zaidi ya watu milioni moja.

Wengi wao ni wafuasi wa Ukristo, hasa wa Kanisa Katoliki (Jimbo Katoliki la Iringa).

Kihistoria Wahehe ni maarufu kwa jinsi walivyopambana na Wajerumani walioteka maeneo yao, k.m. katika pigano la Lugalo mwaka 1891. Kiongozi wao alikuwa Chifu Mkwawa.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Majina ya uko kwiga, mwaluko, Lemanya, mallogo, makome,