Wahaya

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Wahaya ni kabila linalopatikana katika Mkoa wa Kagera, Kaskazini Magharibi mwa Tanzania, kandokando ya Ziwa Victoria. Lugha yao ni Kihaya.

Kabila hilo ndilo linalojulikana kuliko yote ya mkoa wa Kagera, ila ndani yake kuna vijikabila vidogovidogo, kama vile Waziba wa Kiziba, Wahamba wa Muhutwe, Wayoza na waendangabo wa Bugabo, Wanyaiyangilo wa Muleba, Wasubi wa Biharamulo, mfano:- (Kiswahili=Viazi vitamu) = (Kiziba= ebitakuli) = (Kihamba, Kiyoza na Kinyaihangilo = enfuma)

Tofauti kati ya vijikabira zinatambulika kutokana na mabadiliko madogo madogo tu ya maneno na pia lafudhi ya Kihaya ya hiyo sehemu, chakula, ngoma za asili, majina ya asili, n.k.

Flag of Tanzania.svg Makala hii kuhusu utamaduni wa Tanzania bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wahaya kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.