Waberberi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Waberber)
Rukia: urambazaji, tafuta
Maeneo penye wasemaji wa lugha za Kiberberi (Tamazight)

Waberberi ni wakazi asilia wa Afrika ya Kaskazini kuanzia Libya hadi Moroko na nchi za Sahara. Wenyewe wanajiita Amazigh (au: Imazighen) yaani "watu huru". Kabila lao linalojulikana hasa ni Watuareg wanaokalia maeneo ya jangwa kubwa la Sahara.

Leo hii wamepungua kwa sababu wengi wameanza kutumia lugha ya Kiarabu wakihesabiwa kati ya Waarabu.

Wanaoendelea kutumia lugha ya Tamazight (au: Kiberber) kama lugha ya kwanza ni

Katika nchi kavu jangwani au karibu na jangwa maisha yao ni ya ufugaji na kuhamahama. Mlimani walilima. Leo hii ni hasa Watuareg wanaoendelea na maisha ya kuhamahama.

Katika historia wamejulikana tangu mwanzo wa historia kuandikwa. Waroma na Wagiriki wa Kale waliwaita kwa majina kama Wanumidia, Wagaramanti au Walibya.

Kabla ya unenezaji wa Uislamu wengi walikuwa Wakristo na mashuhuri kati hao alikuwa Agostino wa Hippo. Mberberi anayejulikana leo hii ni mchezaji wa mpira Zinédine Zidane.

Viungo vya Nje [hariri]