Wabembe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Wabembe ni kabila la watu ambao wanaishi katika nchi zote za Maziwa Makuu ya Afrika.

Wanapatikana kwa wingi Fizi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na wanaishi katika nchi tofauti kama: Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia, Burundi, Kongo (Brazzaville) na Mkoa wa Kigoma, Tanzania.

Lugha yao ni Kibembe.

Katika mwaka wa 1991 idadi ya Wabembe ilikuwa 252.000 (Kongo, Jamhuri ya Kidemokrasia). Ila kwa sasa idadi ya Wabembe haijulikani kikamilifu, kufuatana na kusambaa kwa kabila hilo kwenye sehemu mbalimbali za mabara tofauti kama vile: Marekani, Australia, Ulaya ya Magharibi na Ulaya ya Kaskazini. Pia idadi ya Wabembe inaongezeka katika nchi za Afrika Kusini, Kenya, Zimbabwe, Malawi na Zambia.

Wabembe wanajiita taifa teule la Mungu kwa sababu wanadai kufanya miujiza ambayo makabila mengine hawawezi kufanya. Wanasema wakati wa vita vijana wao wanakimbia kuliko gari, wanaangusha ndege za maadui kwa mawe, wanakwenda vitani bila silaha na wanashinda.

Ndugu zao ni Warega, Wakongo, Wazimba, Wabangubangu, Wazoba, Wavira na Wangala.

Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Wabembe kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.