Volta ya Juu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Volta ya Juu (Kifaransa: Haute Volta) ilikuwa jina la koloni ya Kifaransa na tangu 1960 nchi huru ya Afrika ya Magharibi inayoitwa Burkina Faso tangu mwaka 1984.
Jina limetokana na mto Volta unaoanza hapa.
Nchi ilianzishwa kwa njia ya kugawa koloni ya Cote d'Ivoire mwaka 1919. Kati ya 1932 na 1947 eneo lake lilitawaliwa na koloni za jirani.
Kiongozi wa nchi Thomas Sankara alibadilisha jina la nchi tar. 4 Agosti 1984.