Vita ya Abushiri

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Vita ya Abushiri ilikuwa jaribio la wenyeji wa pwani la Tanganyika kuzuia utawala wa Kampuni ya Kijerumani kwa Afrika ya Mashariki mwaka 1888/1889 lililokandamizwa na jeshi la Wajerumani. Wajerumani waliita "Uasi wa Waarabu".

Viongozi[hariri | hariri chanzo]

Viongozi wake waliojulikana zaidi walikuwa Abushiri ibn Salim al-Harthi kutoka Pangani na Bwana Heri wa Saadani.

Kufika kwa Wajerumani[hariri | hariri chanzo]

1886 kampuni ilikodisha pwani la Tanganyika kutoka Sultani wa Zanzibar. Mapatano yalianza kutekelezwa Agosti 1888. Wenyeji wa pwani amabo hawakuulizwa wakaona hasara kubadilisha utawala wa Sultani kwa ukali wa kampuni ya Kijerumani.

Pwani la Kaskazini[hariri | hariri chanzo]

Uasi ulianza Pangani ambako wawakilishi Wajerumani walikataza kuonyeshwa kwa bendera ya Sultani na kudai kodi kubwa kwa bidhaa walipojaribu kutumia mamlaka yao. Wananchi waliwakamata na kuwafunga. Waliokolewa na jeshi la Sultani.

Tanga Wajerumani walifungwa pia na kuokolewa na wanajeshi Wajerumani wa manowari ndogo "SMS Moewe".

Tar. 22 Septemba watu wa Bagamoyo walishambulia boma la Wajerumani lakini walizuiliwa na silaha za manowari "Leipzig". Boma iliendelea kushambuliwa.

Pwani la Kusini[hariri | hariri chanzo]

Uasi ulienea katika kusini mnamo 25 Septemba 1888. Maafisa wa kampuni katika Kilwa Kivinje waliuawa. Wajerumani walikimbia kutoka Lindi na Mikindani.

Katika Januari 1889 Wamisionari watatu wakatoliki waliuawa huko Pugu / Dar es Salaam.

Kushindwa kwa kampuni na kuingilia kwa serikali[hariri | hariri chanzo]

Kampuni ilishindwa kukandamiza upizani huu ikaomba serikali ya Berlin kuingilia kati.

Serikali ilichukua koloni mkononi mwaka na wanajeshi kutoka Ujerumani pamoja na wasaidizi wenyeji walikusanyika kwa wengi wakiwa na silaha za kisasa. Kwa jumla makabila wa bara hawakushiriki sana katika vita ya watu wa pwani.

Mwisho wa vita[hariri | hariri chanzo]

Abushiri alikamatwa na kunyongwa tar. 16 Desemba 1889. Bwana Heri alipaswa kujisalimisha. Agosti 1889 vita ilikwisha.

Eeno la awali la kampuni likawa koloni ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani.