Visiwa vya Marshall

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Visiwa vya Marshall

Visiwa vya Marshall ni nchi ya visiwani ya Mikronesia katika Pasifiki ya magharibi.

Nchi jirani katika bahari ni Nauru, Kiribati, Shirikisho la Mikronesia na eneo la Marekani la Kisiwa cha Wake.

Atolli ya Majuro inashika nafasi ya mji mkuu.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Eneo la visiwa vya Marshall ni safu mbili za visiwa au atolli zinazoelea sambamba:

Kwa jumla kuna visiwa na vipande vya atolli 1,150 katika eneo la bahari la km² 1,900,000.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Jina limetokana na nahodha Mwingereza John Marshall aliyetembelea eneo hili mwaka 1788 na kulichora katika ramani. Ingawa visiwa vilikaliwa tayari tangu karne nyingi na watu kutoka Mikronesia lakini jina la Kizungu limebaki kwa ajili ya jumla ya visiwa.

Mwisho wa karne ya 19 Ujerumani ulianzisha ukoloni juu ya visiwa ukaviunganisha kiutawala na Guinea Mpya ya Kijerumani.

Katika vita kuu ya kwanza ya dunia vilitwaliwa na Japani iliyoendelea kutawala visiwa kama eneo lindwa kwa niaba ya Shirikisho la Mataifa.

Baada ya vita kuu ya pili ya dunia vilikuwa chini ya Marekani.

Mwaka 1979 visiwa vimepata madaraka ya kujitawala na hatimaye kupokea uhuru kufuatana na azimio la Umoja wa Mataifa mwaka 1990.

Majaribio ya kinyuklia[hariri | hariri chanzo]

Kuanzia mwaka 1946 Marekani ilitumia visiwa kwa ajili ya majaribio ya mabomu ya nyuklia.

Hadi mwaka 1958 ilitokea milipuko 6,913 kwenye atolli za Bikini na Eniwetok. Hadi leo kuna wakazi wa visiwa wanavyoteswa na maradhi yaliyosababishwa na mnururisho wa mabomu haya. Bikini haitawezekana kukaliwa na watu kabla ya mwaka 2050, Eniwetok haifai kwa makazi ya binadamu kwa miaka 24,000 inayokuja.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi ni 68,000, wengi wakiwa wametokana na wenyeji wa kwanza.

Upande wa dini, wengi ni Wakristo, hasa Wakalvini (51.5%), Wapentekoste, Wakatoliki, mbali ya Wamormoni (8.3%).

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons


Makala hii kuhusu eneo fulani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu eneo hilo kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Je, unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuiongezea habari.


Usitaje majina ya madiwani na viongozi au maafisa wengine wa sasa maana wanabadilika haraka mno.