Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Kilimanjaro (Kilimanjaro International Airport - KIA) kinahudumia eneo la mlima Kilimanjaro pamoja na miji ya Moshi na Arusha katika Tanzania ya kaskazini. .
Ni kiwanja kidogo kinachofikiwa hasa na ndege za Air Tanzania. Makampuni ya kimatifa yanayohudumia KIA ni hasa KLM kutoka Amsterdam na Ethiopian Airlines kutoka Addis Abbaba.
Mwaka 2004 abiria 294.750 walitumia uwanja huu. Hivyo imekuwa kiwanja cha ndege cha pili katika Tanzania baada ya kiwanja cha Dar es Salaam.
[hariri] Makampuni ya Ndege yanayotumia KIA
- Airkenya Express (Nairobi)
- Air Tanzania (Dar es Salaam, Mwanza, Zanzibar)
- Bankair (Zanzibar)
- Condor Airlines (Frankfurt, Mombasa)
- Ethiopian Airlines (Addis Ababa, Dar es Salaam)
- XL Airways
- Kenya Airways (Nairobi, Mombasa)
- KLM Royal Dutch Airlines (Amsterdam, Dar es Salaam)
- Precision Air (Dar es Salaam, Mombasa, Mwanza, Nairobi, Zanzibar)
- Regional Air Services (Tanzania)
- Rwandair Express (Kigali)
- South African Airways (Johannesburg) [imeanza huduma Julai 2007]