Utete

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Utete ni kata ya Wilaya ya Rufiji katika Mkoa wa Pwani, Tanzania, yenye postikodi namba 61601.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi walihesabiwa 6,629 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ilikuwa na wakazi wapatao 5,878 [2] walioishi humo.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Utete ilikuwa makao ya ofisi ya serikali tangu mwaka 1913 ambako serikali ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani iliamua kupeleka hapa makao makuu ya Mkoa wa Rufiji (DOA) kutoka Mohoro [3]. Kabla ya mwaka ule Utete ilikuwa sehemu ya Mkoa wa Kilwa.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. https://www.nbs.go.tz/
  2. "Sensa ya 2012, Pwani - Rufiji DC". Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-03-03. Iliwekwa mnamo 2016-06-18. 
  3. Makala Utete, Muhoro, katika Kamusi ya Koloni za Kijerumani (1920)
Kata za Wilaya ya Rufiji - Mkoa wa Pwani - Tanzania

Chemchem | Chumbi | Ikwiriri | Kipugira | Mbwara | Mgomba | Mkongo | Mohoro | Mwaseni | Ngarambe | Ngorongo | Umwe | Utete


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Pwani bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Utete kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.