Usher Raymond

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Usher)
Rukia: urambazaji, tafuta
Usher
Usher Raymond
Usher Raymond
Maelezo ya awali
Jina la kuzaliwa Usher Raymond IV
Amezaliwa 14 Oktoba 1978 (1978-10-14) (umri 34)
Dallas, Texas
Marekani
Asili yake Chattanooga, Tennessee, Marekani
Atlanta, Georgia
Marekani
Aina ya muziki Pop na R&B
Kazi yake Mwimbaji
Mtunzi wa nyimbo
Mtayarishaji wa rekodi
Mwigizaji
Miaka ya kazi 1994–hadi leo (anaimba)
1998–hadi leo(anaigiza)
Studio LaFace, Arista
Tovuti www.usherworld.com

Usher Raymond IV (amezaliwa tar. 14 Oktoba 1978) ni mwimbaji wa R&B-pop, mtunzi wa nyimbo, na mwigizaji kutoka nchini Marekani. Anafahamika zaidi kwa jina lake la kisanii kama Usher. Usher, alianza kujibebea umaarufu kuanzia miaka ya 1990 hivi. Tangu hapo, ameuza albamu zake takriban milioni 35 kwa hesabu ya dunia nzima na ameshinda Tuzo tano za Grammy.[1]

Mnamo tar. 13 Septemba ya mwaka wa 2008, Usher ameorodheshwa kwenye orodha ya Wasanii Wakali 100 wa Muda Wote na gazeti la Billboard.[2] Ni miongoni mwa wasanii wachache wa lika lake kuorodheshwa katika orodha hiyo. Usher ameanzisha studio yake mwenyewe, inaitwa US Records, na pia ni mmoja kati ya wamiliki wa mradi wa Cleveland Cavaliers.

Yaliyomo

Wasifu [hariri]

Maisha ya awali [hariri]

Usher alizaliwa mnamo tar. 14 Oktoba, katika mwaka wa 1978[3] mjini Dallas, Texas, Marekani.[4] Alizaliwa akiwa kama mtoto wa Bi. Jonetta Patton na Bw. Usher Terry Raymond III;[5] ambao wote ni Wamarekani Weusi.

Alitumia maisha yake yote ya utoto akiwa mjini Chattanooga, Tennessee. Akiwa bwana mdogo, alijiunga na kanisa la kwaya la mtaani alipokuwa akiishi (Chattanooga) na ndipo hapo mama yake alipogundua uwezo wake wa kuimba.[6] Mapema akiwa shule, Usher alijiingiza kwenye mashindano ya kumtafuta mwenye kipaji na kwa bahati nzuri alipata kushinda katika mashindano hayo.

Baadaye famili yake ilihamia mjini Atlanta, Georgia, wakiwa na imani ya kwamba mji huo utakuwa mzuri kwa kukuzia kipaji cha mtoto wao. Wakiwa mjini Atlanta, Usher alijiunga na shule ya North Springs High School.[7]

Maisha binafsi [hariri]

Usher amemwoa Bi. Tameka Foster mnamo mwaka wa 2007,[8] akiwa pamoja naye, wamezaa mtoto wa kiume mmoja aitwaye Usher Raymond V, aliozaliwa mwaka huohuo wa 2007.[9] Mnamo tar. 9 Septemba 2008, ilitangazwa kuwa wawili hao wanategemea kupata mtoto wao mwingine.[10] Mnamo tar. 10 Desemba katika mwaka wa 2008, Foster amezaa mtoto wa pili, aitwaye Naviyd Ely Raymond.[11]

Shughuli za usanii [hariri]

Muziki [hariri]

Filamu [hariri]

  • The Bold And The Beautiful kacheza kama Raymond (1998)
  • The Faculty (1998)
  • She's All That (1999)
  • Light It Up (1999)
  • Texas Rangers (2001) kacheza kama Scipio
  • In the Mix (2005)

Marejeo [hariri]

  1. Grammy Award Winners. The Recording Academy. Rudishwa juu ya 2008-11-17.
  2. The Billboard Hot 100 All-Time Top Artists. Billboard. Nielsen Business Media, Inc. Rudishwa juu ya 2008-11-17.
  3. Usher Raymond - Profile. E!. Rudishwa juu ya 2008-04-26.
  4. Lane, Lynda. Usher: Biography. Allmusic. Rudishwa juu ya 2008-11-18.
  5. Usher: Profile. E!. Rudishwa juu ya 2008-11-18.
  6. Reid, Shaheem. "Usher: King Me", MTV. Retrieved on 2008-11-18. 
  7. North Springs High School. Public School Review. Rudishwa juu ya 2008-11-18.
  8. Finn, Natalie (2007-08-04). Usher Takes the Plunge. E!. Rudishwa juu ya 2008-04-26.
  9. Aswad, Jem (2007-11-28). Usher, Tameka Foster Welcome Baby Boy. MTV. Rudishwa juu ya 2008-01-19.
  10. "Singer Usher and Wife Expecting Second Child", Us, 2008-09-09. Retrieved on 2008-09-11. 
  11. Dyball, Rennie (2008-12-11). Usher Welcomes Baby No. 2. People. Time, Inc. Rudishwa juu ya 2008-12-11.
  12. Usher Says Ne-Yo Will 'Potentially' Work On New Album. MTV.com. Accessed 7 Novemba 2008.

Viungo vya nje [hariri]

Wikiquote-logo.svg
Wikiquote ina mkusanyiko wa dondoo kuhusu:
WikiMedia Commons
Wikimedia Commons ina media kuhusu: