Uqba ibn Nafi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Sanamu la Uqba ibn Nafi huko nchini Algeria

Uqba ibn Nafi (Kiarabu: عقبة بن نافع‘Uqbah ibn Nāfi‘, pia hutajwa kama Oqba ibn Nafi, Uqba bin Nafe, Uqba ibn al Nafia, au Akbah; 622–683) alikuwa jenerali wa jeshi aliyekuwa anatumikia Nasaba ya Wamuawiya, katika vipindi vya Muawiya ibn Abu Sufyan na Yazid ibn Abu Sufyan, ambaye alianza harakati za uenezi wa Uislamu huko Maghrib, ikiwa pamoja na Algeria, Tunisia, Libya na Morocco katika Afrika ya Kaskazini ya leo. Alikuwa mpwa wake 'Amr ibn al-'As. Uqba mara kwa mara huitwa kwa jina la ukoo kama al-Fihri katika kurejelea Banu Fihri, ukoo mmoja uliotokana na kabila la Waquraish. Vizazi vyake vitajulikana kama 'Oqbids' au 'Fihrids'. Uqba ndiye mwanzilishi wa jiji la kitamaduni la Kairouan huko nchini Tunisia.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya Nje[hariri | hariri chanzo]