United Biscuits
United Biscuits (kifupi:"UB") ni kampuni ya kimataifa ya kuunda vyakula :biskuti za BN,biskuti za McVitie's,KP Nuts, Hula Hoops,Kaukau za Real McCoy's, vyakula vya Phineas Fogg, Jacob's Cream Crackers na Twiglets. Kampuni hii iliorodheshwa katika Soko la Hisa la London na ilikuwa mojawapo wa kampuni katika orodha ya FTSE 100 lakini mwezi wa Desemba 2006 ilinunuliwa na kundi la Blackstone na Washirka wa PAI.
Yaliyomo |
[hariri] Historia
United Biscuits ilianzishwa mwaka wa 1948 kutoka kuungana kwa McVitie & Price na Macfarlane Lang.
Mnamo mwaka wa 1972, ilinunua Carr's wa Carlisle ,waliotayarisha biskuti maarufu za Table Water.
Kampuni hii ilimiliki Kampuni ya Wimpy(Mikahawa) kati ya miaka ya 1977 na 1989. Pia ilinunua chakula kampuni ya vyakula baridi ya Ross Young(1988).
Kampuni ilinunuliwa Mei 2000 na Finalrealm,kikundi cha wawekezaji fedha, wakiwa pamoja na Nabisco Holdings Corporation:kama mpango wa biashara Ub ilipewa sehemu ya biashara ya Uropa ya Nabisco.
Kampuni iliuza Young's Bluecrest hapo mwaka wa 2001, ili ienedeshe sekta yake ya biskuti tamu vizuri zaidi.
Mnamo Septemba 2004, kampuni ilinunua sehemu ya Uingereza ya Kundi la Jacob la Biskuti la Groupe Dannone kwa bei ya £ 240 milioni.
Julai 2006,UB iliuza biashara yake ya Kusini mwa Uropa kwa wanunuzi Kraft Foods, ambayo iliacha mmiliki wake na kuanza kujitegemea.
Mnamo Oktoba 2006, Kampuni hii iliuuzwa kwa kundi la Blackstone na Washirika wa PAI. Mpango huo ulikamilika Desemba 2006.
[hariri] Operesheni za UB
Msingi wa biashara hii umo nchini Uingereza,ambapo hupika biskuti na vitafunio vingine chini ya majina mbalimbali yakiwemo: McVitie's na Twiglets.
Kampuni hii ina viwanda vingi katika nchi kadhaa kote Uropa kama vile Uholanzi,Ufaransa na Ubelgiji.
[hariri] Makao makuu
Makao makuu ya kampuni yako Hayes, Middlesex. Kituo kikuu cha usambazaji nchini Uingereza ni kile cha Ashby-de-la-Zouch,hapo pia kuna kiwanda cha kutayarisha vitafunio vya KP.
[hariri] Mfumo wa UB
The 'Mtandao wa UB',ulikuwa ni mtandao wa redio ya kutumikia viwanda vya Uingereza lakini ulifungwa 1979.Ingawaje,mtandao huu ndio ulioanzisha kazi ya mtangazaji maarufu wa redio wa Uingereza Steve Allen na wa televisheni Dale Winton
Tarehe 2 Novemba 2007,[http://en.wikipedia.org/wiki/United_Biscuits#cite_note-10 UB ilitangaza kuwa biskuti zake za Crawford's Bourbon Cream zirudishwe. Sababu ikiwa,kulikuwa na uwezekano wa vipande vidogo vya chuma kuwa ndani ya biskuti.
[hariri] Angalia Pia
[hariri] Marejeo
1 ^ a b "Historia". United Biscuits. http://www.unitedbiscuits.com/about-us.php?rnd=2djB9FgOnxaVmYVMBx3FiTobV4FKJlNRfAt0h2mHW8U%3D.
2. ^ "Bidhaa zetu: Carr's". United Biscuits. http://www.mcvities.com/our-brands.php?rnd=leRc2VgxTHoijbAPt7fcpK9x1Pdbh3mvrcqCTKcPcfE%3D.
3 ^ "Wimpy's",http://www.caterersearch.com/Companies/33925/wimpy-international-ltd.html .
4 ^ ""UB"". Eurofood. Aprili 25, 2002. http://www.findarticles.com/p/articles/mi_m0DQA/is_2002_April_25/ai_85280727.
5 ^ ""United Biscuits kuuza sekta ya Young"". Eurofood. Machi 29, 2001. http://www.findarticles.com/p/articles/mi_m0DQA/is_2001_March_29/ai_73233545.
6 ^ ""Danone yauzia United"". The Independent. July 24, 2004. http://www.findarticles.com/p/articles/mi_qn4158/is_20040724/ai_n12801313.
7 ^ . Telegraph. Julai 11, 2006. http://www.telegraph.co.uk/finance/migrationtemp/2943018/City-sandwich.html.
8 ^ Parkinson, Gary (Oktoba 26, 2006).. The Independent. http://www.findarticles.com/p/articles/mi_qn4158/is_20061026/ai_n16803530.
9 ^ United Biscuits (Desemba 15, 2006). . http://www.unitedbiscuits.com/80256C1A0047922E/vWeb/pcHHUS6WHM5F.
10 ^. BBC. http://www.bbc.co.uk/radio2/shows/pickofthepops/biography.shtml.
11 ^i(2007-11-02), i, http://www.food.gov.uk/enforcement/alerts/2007/nov/bourboncream,
