Falme za Kiarabu
|
|||||
| Wito la taifa: none | |||||
| Wimbo wa taifa: Ishy Bilady | |||||
![]() |
|||||
| Mji mkuu | Abu Dhabi |
||||
| Mji mkubwa nchini | Dubai | ||||
| Lugha rasmi | Kiarabu | ||||
| Serikali | Shirikisho, Ufalme Khalifa bin Zayed Al Nahayan M. bin Rashid Al Maktoum |
||||
| Kuundwa kwa shirikisho |
2 Desemba 1971 | ||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
83,600 km² (ya 116) -- |
||||
| Idadi ya watu - 2005 kadirio - 2005 sensa - Msongamano wa watu |
4,496,000 (ya 116) 4,104,695 [1] 54/km² (ya 143) |
||||
| Fedha | Dirham (AED) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
GMT (UTC+4) +4 (UTC) |
||||
| Intaneti TLD | .ae | ||||
| Kodi ya simu | +971
- |
||||
Falme za Kiarabu (Ar.:الإمارات العربيّة المتّحدة; Ing. United Arab Emirates) ni shirikisho la emirati au falme ndogo 7 katika kaskazini-mashariki ya Rasi ya Uarabuni kwenye mwambao wa ghuba ya Uajemi.
Shirikisho limepakana na Saudia na Omani kwenye nchi kavu; baharini kuna mipaka pia na Katar.
Mji mkuu ni Abu Dhabi na mji mkubwa ni Dubai.
Yaliyomo |
Historia [hariri]
Falme hizo zilikuwa nchi lindwa chini ya Uingereza hadi 1971.
Wakazi [hariri]
Asilimia 80 za wakazi ni wageni, kumbe wenyeji ni sehemu ndogo tu. Zaidi ya nusu ya wageni wanatoka katika nchi za Bara Hindi.
Uchumi [hariri]
Falme za Kiarabu zimekuwa nchi tajiri kutokana na akiba kubwa za mafuta ya petroli. Utajiri huu unapatikana kwa viwango tofautitofauti kati ya emirati zinazozunda shirikisho hili. Abu Dhabi ni emirati mwanachama kubwa ina pia kiasi kikubwa cha petroli na mapato makubwa kutokana na mauzo ya mafuta. Emirati za Dubai na Sharjah zinazalisha pia petroli. Emirati nyingine zinategemea msaada unaotolewa na Abu Dhabi hasa kutokana na mapato yake na pesa hizi zinasaidia ujenzi wa barabara na miundombinu kwa jumla.
Kazi nyingi za ofisini, viwandani, katika biashara na huduma zinatekelezwa na wageni ilhali wenyeji wanashika nafasi ya juu pekee; wengine wasio na vipaji vya kuongoza wanategemea malipo kutoka serikali.
Sheria ya nchi inasema ya kwamba makampuni yote nchini yanapaswa kuwa mkononi mwa raia wazalendo. Hali halisi inamaanisha ya kwamba wageni wanaunda kampuni wakimtafuta mwenyeji anayekubali sehemu ya mali na malipo ya kila mwaka bila kufanya kazi; lakini bila mwenyeji katika uongozi kampuni hairuhusiwi kuendesha shughuli zake kama ni kiwanda, duka au hoteli.
Makampuni kutoka nje yanaweza kupata leseni ya biashara kwa muda katika kanda za pekee bila kumshirikisha mwenyeji.
Falme za shirikisho hili ni:
| Jina | Eneo (km²) | Wakazi mwisho wa 2006 |
|---|---|---|
| Abu Dhabi | 67.340 | 2.563.212 |
| Umm al-Quwain | 777 | 68.000 |
| Fujairah | 1.165 | 130.000 |
| Ras al-Khaimah | 1.684 | 214.000 |
| Sharjah | 2.590 | 699.000 |
| Dubai | 3.885 | 1.327.000 |
| Ajmān | 259 | 258.000 |
Viungo vya nje [hariri]
- (Kiarabu) (Kiingereza) Tovuti ya serikali
- (Kiingereza) UAEInteract.com
| Makala hii kuhusu maeneo ya Asia bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Falme za Kiarabu kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
| Nchi na maeneo ya Asia |
|
Afghanistan | Armenia2 | Azerbaijan | Bahrain | Bangladesh | Bhutan | Brunei | China | Falme za Kiarabu | Georgia2 | Hong Kong3 | Indonesia | Iran | Iraq | Israel | Japan | Kambodia | Kazakhstan | Korea Kaskazini | Korea Kusini | Kupro2 | Kuwait | Kirgizstan | Laos | Lebanon | Macau3 | Malaysia | Maldivi | Mongolia | Myanmar | Nepal | Omani | Pakistan | Palestina | Qatar | Urusi1 | Saudia | Singapore | Sri Lanka | Syria | Taiwan (Jamhuri ya China) | Tajikistan | Timor ya Mashariki | Ufilipino | Uthai | Uturuki1 | Turkmenistan | Uhindi | Uzbekistan | Vietnam | Yemen | Yordani |
| 1. Nchi ina maeneo katika Asia na Ulaya. 2. Nchi hii iko Asia lakini kwa sababu za kihistoria au kiutamaduni inahesabiwa pia kati ya nchi za Ulaya. 3. Eneo la pekee la China. |
