Ulinzi Stars

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Ulinzi Stars ni klabu ya Kenya iliyo na makao yake katika mji wa Nakuru.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Ulinzi Stars ni klabu inayohusishwa na Jeshi la Kenya huku wachezaji wao wengi wakiwa wanajeshi. Wao hushindana katika ngazi ya juu ya ligi, Ligi Kuu ya Kenya. Timu hii imekuwa mabingwa wa Kenya mara tatu; mwaka wa 2003,wa 2004, na wa 2005 . Hii ilifanya kuwa timu ya tatu katika Ligi Kuu ya Kenya kuwa mabingwa kwa miaka mitatu mfululizo, baada ya AFC Leopards na Gör Mahia. Ulinzi Stars hucheza mechi zao katika Uwanja wa Afraha,[Nakuru]. Hapo zamani, makao ya klabu hiyo ilikuwa katika mji wa [Thika], lakini imehamia mji wa [Nakuru] tangu msimu wa 2004/05.Mechi zao zote za nyumbani wamekuwa wakicheza katika Uwanja wa Afraha, [Nakuru].

Ulinzi Stars pia ndio timu ya Jeshi La Kenya na wamehitimu kucheza katika Mashindano Ya Majeshi Duniani ya mwaka wa 2011.

Mbali na kuwa na timu ya soka,walikuwa na timu ya mpira wa vikapu iliyoitwa Ulinzi Warriors.Ulinzi Warriors iliacha kucheza mwaka wa 2007 ingawa walikuwa Mabingwa watetezi katika ligi ya mpira wa vikapu.Timu hii ilikuwa imeshinda ligi hiyo ya mpira wa vikapu mara tano mfululizo.Palikuwepo pia na timu za raga na voliboli.

Utendaji katika mashindano ya CAF.[hariri | hariri chanzo]

Ligi ya Mabingwa ya CAF 2004: Ilijitoa katika raundi ya kwanza

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]