Ukambani
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Ukambani ni sehemu ya kusini ya Mkoa wa Mashariki nchini Kenya. Inakaliwa na Wakamba.
Eneo la Ukambani laanza upande wa mashariki wa Nairobi na kuendelea hadi Voi; kwa mtazamo tofauti ni eneo kati ya Embu na mpaka wa Tanzania.
Mazingira yake huona ukame wa mara kwa mara pamoja na njaa inayokuja sambamba nayo.
Wilaya za Ukambani ni hasa Machakos, Makueni, Kitui, Makueni na Mwingi.