Ufizi wa meno

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nafasi ya ufizi wa meno katika muundo wa jino

Ufizi wa meno (lat. gingiva; ing. gum) ni tishu laini inayofunika mataya ndani ya kinywa.

Inaziba hasa nafasi kati ya kizizi cha jino na kitundu cha taya.

Tofauti na tishu laini ya midomo na mashavu ufizi unashikana na mfupa wa mataya chini yake.

Ufizi ulio mzima unaonyesha kwa kawaida rangi ya waridi lakini kwa watu wenye ngozi nyeusinyeusi inaweza kuwa pia na kiwango cha melanini. Kutokea kwa madoa nyekundu, nyeupe na buluu ni alama ya magonjwa yanayohitaji kuangaliwa na daktari wa meno.