Turibio wa Mongrovejo
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtakatifu Turibio wa Mongrovejo (16 Novemba, 1538 – 23 Machi, 1606) alikuwa askofu nchini Peru. Ametambuliwa kuwa mtakatifu. Tarehe ya kifo chake, yaani 23 Machi pia ni sikukuu yake.
[hariri] Maisha
Turibio wa Mongrovejo alizaliwa nchini Hispania mnamo mwaka wa 1538. Alijifunza sheria huko Salamanka, na mwaka wa 1580 aliteuliwa kuwa Askofu wa Lima nchini Peru, akaenda Amerika. Alikuwa motomoto kwa kazi za kitume, akiitisha mikutano mbalimbali ili kurekebisha mambo ya dini katika nchi nzima. Kwa nguvu zote alitetea haki za kanisa, aliwatembelea Wakristo waliokuwa chini yake, na kufanya kazi kwa muda mrefu kwa mafaa ya wenyeji wa Peru. Alikufa mwaka wa 1606.
[hariri] Tazama pia
[hariri] Marejeo
- "Sala ya Kanisa - Vipindi vya Liturjia", Toleo la Tatu 1996, Ndanda - Peramiho: Benedictine Publications, uk.1311
| Makala hii kuhusu Mkristo huyu bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Turibio wa Mongrovejo kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |