Tufani
Kutoka Wikipedia
Tufani ni dhoruba yenye mwendo wa kuzunguka. Inasababishwa na eneo la shindikizo duni la hewa ambako upepo imeanza kuzunguka ndani yake.
Mzunguko huu hufuata mwendo wa saa katika maeneo kusini ya ikweta na huenda kinyume cha mwendo wa saa katika maeneo kaskazini ya ikweta.
[hariri] Chamchela na Kimbunga
Tufani ikitokea kwenye nchi kavu huitwa chamchela.
Kwenye bahari za tropiki mzunguko unaongezeka nguvu kutoka nishati ya joto ya maji baharini kuwa dhoruba kali. Tufani hizi zinazoanza baharini huitwa kimbunga. Kimataifa kuna majina mengine yaliyo tofauti kila bahari kama vile:
- Katika eneo la Atlantiki (Karibi hasa) kimbunga huitwa hurikan (kiing. Hurricane)
- katika eno la Pasifiki kimbunga huitwa taifuni (en:typhoon)
- katika eneo la Bahari Hindi na penginepo jina la saikloni (en:cyclone) limetumiwa mara nyingi
[hariri] Tufani katika anga ya nje
Tufani zimetazamiwa pia katika falaki kwenye sayari za mfumo wa jua letu kama Mshtarii na Meriki. Hasa doa nyekundu kubwa lililoonekana kwenye Mshtarii tangu miaka 178 limetambuliwa kuwa tufani.
| Makala hiyo kuhusu "Tufani" bado ni mbegu. Unaweza kusaidia kuikuza kwa kubofya kitufe kilichoandikwa "hariri". Ikiwepo makala kuhusu Tufani kwa lugha nyingine, unaweza kuitafsiri kwa Kiswahili. |


