Trinidad na Tobago

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Trinidad)
Republic of Trinidad and Tobago
Bendera ya Trinidad na Tobago Nembo ya Trinidad na Tobago
Bendera Nembo
Kaulimbiu ya taifa: Together we aspire, together we achieve
Wimbo wa taifa: Forged From The Love of Liberty
Lokeshen ya Trinidad na Tobago
Mji mkuu Port of Spain
10°40′ N 61°31′ W
Mji mkubwa Chaguanas [1]
Lugha rasmi Kiingereza
Serikali Jamhuri
Paula-Mae Weekes
Keith Rowley
Uhuru
Kutoka Uingereza

31 Agosti 1962
Eneo
 - Jumla
 - Maji (%)
 
5,131 km² (ya 165)
Kidogo sana
Idadi ya watu
 - Julai 2019 kadirio
 - Msongamano wa watu
 
1,363,985 (ya 151)
264/km² (ya 54)
Fedha Trinidad and Tobago dollar (TTD)
Saa za eneo
 - Kiangazi (DST)
(UTC-4)
(UTC n/a)
Intaneti TLD .tt
Kodi ya simu +1-868

-


Jamhuri ya Trinidad na Tobago ni nchi ya visiwani katika Karibi ya kusini, karibu na pwani ya Venezuela, kusini kwa kisiwa cha Grenada cha Antili Ndogo. Nchi jirani nyingine kuvukia bahari ni Barbados na Guyana.

Nchi ina eneo la km² 5,128 ambalo karibu lote ni kisiwa kikuu cha Trinidad. Kile cha Tobago kina asilimia 6 tu za eneo pamoja na 4% ya wakazi. Kuna visiwa vidogo vingine 21.

Ni jamhuri mwanachama wa Jumuiya ya Madola.

Ni nchi iliyoendelea, ikishika nafasi ya tatu kati ya zile za Amerika baada ya Marekani na Kanada.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Visiwa vilikaliwa na Waindio kwa karne nyingi kabla ya ujio wa Kristofa Columbus na Wahispania (1498).

Trinidad ilibaki chini ya wakoloni hao hadi mwaka 1797 vilipotekwa na Waingereza ambao walikabidhiwa pia Tobago mwaka 1802. Viliunganishwa mwaka 1889 na kubaki koloni hadi mwaka 1962 vilipopata uhuru.

Mwaka 1976 nchi imeanza kuwa jamhuri.

Watu[hariri | hariri chanzo]

Wakazi wengi wana asili ya India (37.6%), lakini pia ya Afrika (36.3%) na sehemu nyingine. Hivyo kuna machotara wa aina mbalimbali (24.2%).

Lugha rasmi ni Kiingereza, lakini wananchi wengi wanaongea kwa kawaida aina mbili za Krioli. Asilimia 5 wanaongea Kihispania.

Upande wa dini wengi (63%) ni Wakristo wa madhehebu mbalimbali, kuanzia Kanisa Katoliki (21.5%), Wapentekoste (12%) na Anglikana (5.7%). Wahindu ni 18% na Waislamu ni 5%.

Tazama pia[hariri | hariri chanzo]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

WikiMedia Commons
WikiMedia Commons
Makala hii kuhusu maeneo ya Bahari ya Karibi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Trinidad na Tobago kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.