Toni Morrison

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Toni Morrison

Amezaliwa Chloe Ardelia Wofford
18 Februari 1931
Ohio, Marekani
Amekufa 5 Agosti 2019
New York City
Nchi Marekani
Kazi yake Mwandishi

Toni Morrison (18 Februari 19315 Agosti 2019) alikuwa mwandishi wa kike nchini Marekani na mshindi wa Tuzo ya Nobel ya Fasihi ya mwaka 1993.

Alizaliwa kwa jina la Chloe Anthony Wofford tarehe 18 Februari 1931 huko Lorain, Ohio - 2019 kama mtoto wa pili wa familia ya Waamerika weusi. Wazazi wake walikuwa wafanyakazi.

Alipenda kusoma vitabu tangu utoto. 1949 akajiunga na chuo kikuu cha Howard (chuo kwa Waamerika weusi katika mji mkuu Washington D.C.) akimaliza kwa digrii ya BA katika somo la Kiingereza. Wakati ule aliacha jina lake la Chloe akatumia "Toni" kama kifupi cha "Anthony". Mwaka 1955 alipata MA (shahada ya pili) kutoka chuo kikuu cha Cornell.

Alianza kufundisha fasihi kwenye chuo kikuu cha Texas Kusini mjini Houston, tangu 1957 tena Howard. Aliolewa na Howard Morrison akazaa watoto wawili. Baada ya talaka mwaka 1964 alianza kazi ya uhariri wa vitabu kwa wachapishaji wa Random House. Alihariri vitabu vingi vya waandishi weusi.

Mwaka 1970 alitoa kitabu chake cha kwanza "The Bluest Eye" (Jicho la buluu kabisa). Kitabu cha kwanza kilichofaulu kuuzwa vema kilikuwa "Song of Solomon" (Wimbo ya Suleimani) mwaka 1977. Mwaka wa 1988 alituzwa Tuzo ya Pulitzer ya Bunilizi kwa riwaya yake Beloved.

Tangu 1989 amefundisha kama profesa katika chuo kikuu cha Princeton. 1993 alipokea Tuzo ya Nobel ya Fasihi.

Kati ya riwaya zake ni:

  • The Bluest Eye, 1970
  • Sula, 1973
  • Song of Solomon, 1977
  • Tar Baby, 1981,
  • Beloved, 1987
  • Jazz, 1992
  • Paradise, 1998
  • Love, 2003


Makala hii kuhusu mwandishi fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Toni Morrison kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.