Togwa
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Togwa ni kinywaji baridi kinachotengenezwa kwa nafaka au maji ya matunda. Namna ya kutengeneza ni sawa na pombe ya kawaida ila tu haikubadilika bado kuwa na alikoholi.
Togwa ndiyo itakuwa pombe ikikaa. Kwa mfano, togwa ya ulanzi ni utomvu kutoka mianzi baada ya masaa kadhaa, na ulanzi wenye pombe ni utomvu uleule kutoka mianzi baada ya siku mbili hivi.
Nafaka zinazotumika kutengenezea zaidi huwa ni mtama au mahindi.
Jinsi ya kutengeneza togwa la mtama [hariri]
Chemsha mtama mpaka uive kama uji, halafu uvumbike kwa siku mbili tia sukari ni tayari kwa kunywewa.
| Makala hii kuhusu mambo ya utamaduni bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Togwa kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |