Mambo Huangamia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Things Fall Apart)

Mambo Huangamia (kwa Kiingereza "Things Fall Apart") ni riwaya iliyoandikwa na Chinua Achebe.

Kitabu hicho alichokiandika mwishoni mwa miaka ya 1950 kilitolewa mwaka wa 1958 na kumpatia jina kubwa duniani. Hicho, kinaaminika ndicho kitabu chake bora zaidi, ni kitabu kilichosomwa kwa wingi zaidi katika vitabu vya tamthiliya ya Kiafrika.[1]

Hadithi ya riwaya hii imefuatiwa na Hakuna Starehe Tena (1960) na Mshale wa Mungu (1964).

Mkondo wa hadithi[hariri | hariri chanzo]

Mhusika mkuu anaitwa Okonkwo, tajiri katika kijiji cha Umuofia. Huyo Okonkwo hufuata vizuri sana mila na desturi za Waigbo ili kumshinda baba yake ambaye ni duni.

Katika kufuata hizo mila alifika hatua ya kumuua mwana wake wa kambo na wanakijiji wakakubali. Siku moja, lakini, Okonkwo kwa bahati mbaya alimuua mwanakijiji mwingine akahukumiwa kuondoka kijijini kwake kwa miaka saba zinavyoamuru mila za kijiji.

Huko uhamishoni Okonkwo alikutana na wamisionari Wazungu, akasikitika sana kugundua mwana wake mwenyewe aliacha mila za Kiigbo na kukubali dini ya Ukristo.

Okonkwo akirudi kijijini baadaye akakuta hata maisha ya kijijini yameathiriwa na hiyo dini mpya. Akaanza kuupiga vita Ukristo, hatimaye lakini aliona kuwa haiwezekani kurudi kwa maisha ya kimila akajiua kwa kujinyonga.

Tanbihi[hariri | hariri chanzo]

  1. Franklin, Ruth. "After Empire: Chinua Achebe and the Great African Novel". The New Yorker, 26 May 2008. Retrieved 7 December 2010.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  • (de) "Kindlers Literaturlexikon" (1970), diwani ya 10, Zürich: Kindler, uk.9345
Makala hii kuhusu kitabu fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Mambo Huangamia kama Mwandishi wake, hadithi au matoleo yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.