The O.C.
| The O.C. | |
|---|---|
![]() Nembo ya The O.C. |
|
| Aina | Maigizo ya vijana |
| Imetungwa na | Josh Schwartz |
| Imeongozwa | Dave Bartis (season 1) Bob DeLaurentis Doug Liman (season 1) McG Stephanie Savage (season 4; co-executive producer seasons 1–3) Josh Schwartz |
| Nchi inayotoka | Marekani |
| Lugha | Kiingereza |
| Ina misimu | 4 |
| Ina sehemu | Orange County, California |
| Utayarishaji | |
| Sehemu | Orange County, California |
| Muda | makisio ni dk. 42 |
| Urushaji wa matangazo | |
| Kituo | Fox |
| Inarushwa na | 5 Agosti, 2003 |
The O.C. ni kipindi cha Marekani kilichohusu maisha ya vijana iliyoonyeshwa kuanzia Agosti 5, 2003 hadi Februari 22, 2007 kwenye Stesheni ya Fox Broadcasting Company. Kipindi hiki, kilichobuniwa na Josh Schwartz, kinahusu maisha ya kundi la vijana na familia zao wanapoishi mtaani Newport Beach kwenye mji wa Orange County, California.
The O.C. imeonyeshwa kwenye zaidi ya nchi 50 kote duniani na ilikuwa mojawapo ya vipindi maarufu mnamo 2003.[1] The O.C. ilivutia watazamaji milioni 9.7 katika msimu wake wa kwanza, lakini watazamaji walianza kupungua katika misimu iliyofuatia.
Yaliyomo |
[hariri] Stesheni zilizoonyesha kipindi hiki
Msimu wa kwanza ulianza saa tatu jioni mnamo Agosti 5, 2003 kwenye stesheni ya Fox nchini Marekani. Pia, ilionyeshwa nchini Canada kwenye stesheni ya CTV.[2][3]
Nchini Uingereza, kipindi cha kwanza kilianza mnamo Machi 7, 2004 saa tatu usiku kwenye stesheni ya Channel 4.[4]
Nchini New Zealand, kipindi hiki kilionyeshwa kwenye stesheni ya TG4.[5]
Nchini Afrika Kusini, ilianza Aprili 1, 2004 kwenye stesheni ya Go.[6]
[hariri] Wahusika Wakuu
- Peter Gallagher aliigiza kama Sandy Cohen, ambaye ni wakili, babake Seth na mumewe Kristen Cohen. Yeye anafungua ofisi yake ya kibinafsi na ni meneja. Mwishowe wa kipindi hiki, anakuwa profesa kwenye chuo cha Berkeley.
- Kelly Rowan aliigiza kama Kristen Cohen. Yeye ni mkewe Sandy, na mamake Seth. Kabla ya kukutana na Sandy, yeye alipendana na Jimmy Cooper. Amewahi kupata shida ya kulewa.Baadaye, anakuwa mjamzito na mtoto huyo anaitwa Sophie Rose Cohen.
- Benjamin McKenzie aliigiza kama Ryan Atwood, ambaye ni kijana matata. Mamake alimfukuza nyumbani, na baadaye anachukuliwa na Sandy Cohen kulelewa. Ryan anapendana na Marissa, lakini uhiusiano wao ulipata pandashuka tele. Mwishowe, Ryan na Marissa wanapata ajali barabarani na Marissa anakufa mikononi mwake.
- Mischa Barton aliigiza kama Marissa Cooper, mpenzi wa Ryan. Yeye ni rafiki wa dhati wa Summer. Yeye pia amepata pandashuka nyingi, kama matumizi yamadawa ya kulevya.
- Adam Brody aliigiza kama Seth Cohen. Yeye ni mpenzi wa Summer. Baadaye, anamuoa Summer.
- Rachel Bilson aliigiza kama Summer Roberts, mpenzi wa Seth. Yeye ni mwana wa Dkt. Neil Roberts.
[hariri] Mafanikio
| Msimu | Vipindi | Saa | Mwanzo wa msimu | Mwisho wa msimu | Mwaka | Namba | Watazamaji (milioni) |
|---|---|---|---|---|---|---|---|
| 1 | 27 | Jumanne saa 9:00 jioni (2003) Jumatano saa 9:00 jioni (2003–04) |
Agosti 5, 2003 | Mei 5, 2004 | 2003–04 | #57 | 9.7[7] |
| 2 | 24 | Alhamisi 8:00 p.m. | Novemba 4, 2004 | Mei 19, 2005 | 2004–05 | #85 | 7.0[8] |
| 3 | 25 | Alhamisi saa 8:00 jioni (2005) Alhamisi saa 9:00 jioni (2006) |
Septemba 8, 2005 | Mei 18, 2006 | 2005–06 | #105 | 5.6[9] |
| 4 | 16 | Alhamisi saa 9:00 jioni | Novemba 2, 2006 | Februari 22, 2007 | 2006–07 | #123 | 4.3[10] |
[hariri] Tuzo
[hariri] Logie Awards
- Mnamo 2005, The O.C ilisinda tuzo la Most Popular Overseas Program.
[hariri] PRISM Awards
- Mnamo 2006, muigizaji Kelly Rowan alishinda tuzo la Performance in a TV Drama Series Episode.
[hariri] Teen Choice Award
- Mnamo 2004, Mischa Barton alishinda tuzo la Choice Breakout TV Star - Female.
- Mwaka huo huo, Adam Brody pia alishinda tuzo la Choice TV Actor - Drama/Action Adventure.
- Mwaka wa 2005, Rachel Bilson alishinda tuzo la Choice TV Actress:Drama.[11]
[hariri] Marejeo
- ↑ Associated Press. "Fox's once hot 'The O.C.' canceled", Regina Leader-Post, January 5, 2007. Retrieved on February 10, 2007.
- ↑ McFarland, Melanie (August 5, 2003). Fox's handsome 'The O.C.' may be just what teens crave. Seattle Post-Intelligencer. Hearst Corporation. Rudishwa juu ya January 24, 2009.
- ↑ Gee, Dana. "Daring to do good: Role in the O.C. Peter Gallagher feels close to his", The Gazette, CanWest Interactive, August 2, 2003. Retrieved on February 9, 2009.
- ↑ Clark, Caren. "Switched on this week the best bits on TV", Southport Reporter, PCBT Photography, March 6, 2004. Retrieved on July 16, 2008.
- ↑ Kenny, Colum (August 27, 2006). Time to call a halt to the lip service behind TG4 'success'. Irish Independent. Rudishwa juu ya 2009-09-14.
- ↑ The O.C.. TVSA. Rudishwa juu ya 2009-09-14.
- ↑ I. T. R. S. Ranking Report: 01 Thru 210. ABC Medianet. Archived from the original on September 30, 2007. Rudishwa juu ya May 25, 2007.
- ↑ Primetime series. The Hollywood Reporter. Nielsen Business Media (May 27, 2005). Rudishwa juu ya September 12, 2009.
- ↑ Series. The Hollywood Reporter. Nielsen Business Media (May 26, 2006). Rudishwa juu ya September 12, 2009.
- ↑ 2006–07 primetime wrap. The Hollywood Reporter. Nielsen Business Media (May 25, 2007). Rudishwa juu ya June 19, 2009.
- ↑ "The Teen Choice Awards – Nominees", 20th Century Fox, 2005. Retrieved on August 14, 2008.
