Tasmania

Kutoka Wikipedia

Tasmania katika Australia
Tasmania katika Australia
Bandari ya Hobart
Bandari ya Hobart

Tasmania ni kisiwa kikubwa upande wa kusini wa Australia bara ni jimbo la Australia lenye eno la 90,758 km². Mji mkuu pia mji mkubwa kisiwani ni Hobart.

[hariri] Wenyeji asilia

Wataalamu huamini ya kwamba Tasmania ilikuwa sehemu ya bara la Australia hadi miaka 12,000 iliyopita. Wakati ule watu wameshafika kisiwani lakini kutokea kwa mlango wa bahari kuliwatenga na wenyeji wa Australia. Hiyvo walikosa mawasiliano na watu wengine wakaendelea na teknolojia isiyoendelea. Wakati wa kufika kwa Wazungu katika karne ya 17 wenyeji walikuwa na vifaa vichache vya ubao na mawe tu lakini hawakuwa na pinde na mishale, hawakuvua kwa nyavu, hawakujua mashua wala kufuga wanyama au kulima.

[hariri] Historia ya kikoloni

Tasmania ilifikiwa na Mholanzi Abel Tasman mwaka 1642 na kupewa jina la "Van-Diemens-Land". Tangu 1803 Uingereza ilivamia kisiwa na kuitumia kama gereza kwa wafungwa kutoka Uingereza au Australia. Walowezi na wafugaji wa kondoo walikuja pia.

Wenyeji asilia waliuawa kwa wingi hadi kupotea kabisa. Leo kuna tu wajukuu wa wanawake wenyeji waliokamatwa na Wazungu na kuzaa nao.

[hariri] Wakazi

Leo hii kuna takriban watu nusu milioni kisiwani.

Vifaa binafsi