Tashtiti

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru

Tashtiti (kwa Kiing. rhetorical question) ni mbinu ya kuuliza swali kwa jambo ambalo unafahamu jibu lake, na hufanya hivyo kwa lengo la kusisitiza jambo, kuleta mshangao, n.k.

Mfano
  • Ikiwa mtu kapoteana na rafiki yake kwa muda mrefu, halafu ghafla wanakutana, huweza kumwuliza "Aisee! ni wewe?", hali anajua kuwa ni yeye.

Tashtiti katika fasihi

Katika fasihi tashtiti (kiing. satire) ni mbinu unaolenga kukosoa maovu, ujinga, unyanyasaji na kasoro kwa namna ya kejeli au utani, mara nyingi kwa shabaha ya kuhamasisha maboresho.

Mara nyingi aina mbili za tashtiti hutofautishwa zinazolinganishwa na mbinu tofauti za wanatashtiti Horatius na Juvenal wa Roma ya Kale.

Tashtiti ni mbinu ambayo imetumiwa na watunzi kutaja yasiyotajika bila kuchukiza, kuchukuliwa vibaya au kumuudhi msomaji. Tashtiti huwasilisha maudhui nyeti kwa njia ya ucheshi. Tashtiti haiibui tu ucheshi bali ni ucheshi wenye lengo la kurekebisha.[1]

Tanbihi

  1. Ayodi, Beja, Ogola: Tashtiti na Wanatashtiti, maana, umuhimu na vipengele vyake katika fasiki; Mulika na. 33, uk. 46-57

Marejeo