Supamaketi za Uchumi

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Supamaketi za Uchumi
Ilipoanzishwa 1975
Makao Makuu Nairobi
Tovuti [1]

Supamaketi za Uchumi ni mtandao wa supamaketi hapa Kenya ulioanzishwa mwaka wa 1975 na uliorodheshwa katika soko la hisa la Nairobi katika mwaka wa 1992. [1]

Kufungwa na kufunguliwa tena[hariri | hariri chanzo]

Uchumi ilifungwa, kwa muda, katika mwezi wa Juni 2006 baada ya miaka 30 ya biashara. [2] Wakati huo kufungwa kwake kulionekana kama msiba mkubwa zaidi uliokumba biashara katika historia ya Kenya. [3] Baadaye serikali ilianzisha mpango wa kuiokoa na hapo basi vituo tano vya Uchumi vikafunguliwa tena tarehe 15 Julai 2006 vyote vikiwa katika Nairobi.

Hivi Sasa[hariri | hariri chanzo]

Wakati wa Januari 2011 Uchumi imeendesha maduka 17 nchini Kenya na 1 nchini Uganda. Duka jipya linapangwa kufungua mjini Daressalaam mwaka 2011, nyingine katika miaka ijayo huko Juba, Sudan Kusini. [4] Kampuni ina wenye hisa 12,000 wanaosubiri kurudishwa kwa kampun kwenye soko la hisa la Nairobi.[5]

Angalia pia[hariri | hariri chanzo]

  • Nakumatt, mshindani wa Uchumi nchini Kenya

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

</references>Kigezo:Retail-stub
Cite error: <ref> tags exist, but no <references/> tag was found