Hispania
|
|||||
| Wito la taifa: Plus Ultra (Kilatini kwa "Mbele na zaidi") |
|||||
| Wimbo wa taifa: Marcha Real au Marcha Granadera | |||||
![]() |
|||||
| Mji mkuu | Madrid |
||||
| Mji mkubwa nchini | Madrid | ||||
| Lugha rasmi | Kihispania(1) | ||||
| Serikali | Ufalme wa kikatiba Juan Carlos I José Luis Rodríguez Zapatero |
||||
| Kuungana kwa nchi Kungana kwa ndoa za wafalme Maungano Hali halisi Kisheria |
1516 1716 1812 |
||||
| Eneo - Jumla - Maji (%) |
504,782 km² (ya 50) 1.04% |
||||
| Idadi ya watu - 2006 kadirio - 2001 sensa - Msongamano wa watu |
44.395.286 (ya 29) 40,847,371 87.8/km² (ya 106) |
||||
| Fedha | Euro (€)(2) (EUR) |
||||
| Saa za eneo - Kiangazi (DST) |
CETKigezo:Footnote (UTC+1) CEST (UTC+2) |
||||
| Intaneti TLD | .es | ||||
| Kodi ya simu | +34
- |
||||
| Kigezo:Fnb Majimbo ya kujitawala ya Hispania yanatumia lugha za: Kikatalan/Kivalencia, Kibaski na Kigalicia pamoja na Kihispania. Katika Bonde la Val d'Aran lahaja ya Kiarani ya lugha ya Kioksitani ni lugha rasmi pamoja na Kihispania; Kigezo:Fnb Hadi 1999: Peseta Kigezo:Fnb Ispokuwa Visiwa vya Kanari |
|||||
Hispania ni nchi ya Ulaya ya kusini-magharibi. Imepakana na Ufaransa, Andorra, Ureno na eneo la Kiingereza la Gibraltar. Kuna pwani ndefu ya Bahari ya Mediteranea na pia ya Atlantiki. Visiwa vya Baleari kwenye Mediteranea na Visiwa vya Kanari katika Atlantiki pamoja na miji ya Afrika ya Kaskazini Ceuta na Melilla ni sehemu za Hispania.
Hispania bara ni sehemu kubwa ya rasi ya Iberia. Mji mkuu ni Madrid ambayo ni pia mji mkubwa wa nchi. Eneo la nchi ni 500,000 km² ambalo lina wakazi 44.395.286 (2006).
Lugha rasmi ni Kihispania lakini majimbo 17 yamepewa mamlaka ya kujitawala katika mambo mbalimbali pamoja na siasa ya kiutamaduni hivyo lugha za Kikatalan, Kivalencia, Kibaski na Kigalicia zimekuwa lugha rasmi za kijimbo pamoja na Kihispania. Wahispania walio wengi ni waamini wa Kanisa Katoliki.
Muundo wa serikali ni Ufalme wa Kikatiba. Mfalme Juan Carlos I amevaa taji tangu mwaka 1978. Anaheshimiwa sana kwa sababu aliongoza taifa katika mabadiliko ya kutoka udikteta wa jenerali Francisco Franco kuelekea demokrasia. Hasa tendo la mfalme la kuzuia mapinduzi wa kijeshi linakumbukwa sana. Lakini kisheria madaraka yake ni madogo.
Utawala umo mikononi mwa serikali inayochaguliwa na bunge linaloitwa "Las Cortes likichaguliwa kwa kura za kidemokrasia.
Yaliyomo |
Historia[hariri]
Historia ya awali[hariri]
Wakazi wa kwanza waliojulikana kwa jina kuwa waliishi Hispania walikuwa Wakelti. Katika karne za 1 KK Wafoinike walianzisha miji kwenye pwani na kuchimba madini hasa shaba na fedha.
Waroma[hariri]
Waroma wa Kale walivamia na kutawala Hispania kwa karne kadhaa wakileta lugha yao ya Kilatini kilichopata kuwa msingi wa lugha za kisasa za Hispania. Kibaski pekee si lugha ya Kirumi.
Katika karne ya tano makabila ya Kigermanik walivamia Dola la Roma pamoja na Hispania. Wavandali na Wavisigothi walitawala sehemu kubwa ya Hispania.
Waarabu[hariri]
Tangu mwaka 711 jeshi la Waarabu Waislamu liliingia kutoka Afrika ya Kaskazini na kutwaa sehemu kubwa ya Hispania hadi karibu milima ya Pirenei lakini watawala wa maeneo kadhaa katika kaskazini walijihami na kufaulu kudumisha uhuru wao. Waarabu walileta fani nyingi za maendeleo nchini.
Katika kipindi cha vita cha karne nyingi Wakristo wa Kaskazini walifaulu polepole kuwarudisha nyuma Waarabu hadi kusini ya nchi.
Mwaka 1492 mfalme Boabdil wa Granada mji wa mwisho wa Waarabu alishindwa na mfalme Ferdinand II wa Aragon na malkia Isabella wa Kastilia.
Makoloni ya Amerika[hariri]
Wiki chache kabla ya kushinda huko Granada wafalme wa Hispania walimkubali nahodha Kristoforo Kolumbus na kumpa kibali cha kutafuta njia ya kufika Bara Hindi kupitia magharibi. Badala ya kufika India Kolumbus alifika kwenye visiwa vya Amerika ya Kati.
Huo ulikuwa mwanzo wa upanuzi wa Hispania katika "Dunia Mpya" ya Amerika. Wahispania walijenga dola kubwa la kikoloni na kutwaa karibu Amerika ya Kusini yote pamoja na Amerika ya Kati na Mexiko hadi sehemu za kusini za Marekani ya leo.
Katika miaka mia tatu iliyofuata Hispania ilitajirika sana kutokana na maliasili ya Amerika.
(ya kuendelea)
Jiografia[hariri]
Miji mikubwa[hariri]
- Madrid ni mji mkuu - wakazi 3,200,000.
- Barcelona - wakazi 1,600,000
- Valencia - wakazi 800,000.
- Seville - wakazi 705,000.
- Zaragoza katika Aragon- wakazi 650,000.
- Malaga katika Andalucia - wakazi 560,000.
- Murcia katika bonde la Segura - wakazi 410,000.
- Las Palmas de Gran Canaria ni mji mkuu wa Visiwa vya Kanari - wakazi 378,000.
- Palma de Mallorca kwenye Visiwa vya Baleari - wakazi 375,000.
- Bilbao ya Ubaski katika kaskazini - wakazi 350,000.
Picha za Hispania[hariri]
-
Daraja lililojengwa zamani za Dola la Roma huko Cordoba
-
Kanisa la Sagrada Familia mjini Barcelona
-
Mlima wa Alto de Angliru
-
Kisiwa cha Deva inavyoonekana kutoka Rasi Vidrias
| Makala hii kuhusu maeneo ya Hispania bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Hispania kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |
|
||||||||||||||
