Siwa barafu
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Siwa barafu ni kipande kikubwa cha barafu kinachoelea baharini.
[hariri] Asili ya siwa barafu
Kwa kawaida siwa barafu hupatikana kama vipande vinavunjika kwenye barafuto au maganda ya barafu nchani na kuanguka kwenye maji ya bahari.
[hariri] Tabia
Barafu ni nyepesi kushinda maji na hivyo kipande cha barafu kitaelea kwenye maji lakini sehemu kubwa ya siwa barafu iko chini ya maji.
Siwa barafu huelea pamoja na mwendo wa mikondo ya bahari. Kadiri inavyofika kwenye maji yasiyo baridi tena muda wa maisha ni miezi hadi miaka kadhaa. Muda huu hadi kuyeyuka kabisa unategemea ukubwa wa siwa barafu na halijoto ya eneo inapofika. Zimetazamiwa kwa muda wa miaka 3.
Mara nyingi zinaonekana mita 1 hadi 75 juu ya uso wa bahari; uzito hufikia hadi tani 100,000 au 200,000. Siwa barafu kubwa katika Atlantiki ya kaskazini iliyotazamiwa ilikuwa na mita 168 juu ya maji yaani kimo cha nyumba ya ghorofa 55.
[hariri] Hatari kwa meli
Siwa barafu ni hatari kwa meli kwa sababu sehemu kubwa iko chini ya maji ni asilimia 10 pekee inaonekana juu ya uso wa bahari. Kama meli inakaribia mno kuna uwezekano ya kwamba siwa barafu iko chini ya maji mita mamia kutoka kilele chake kinachoonekana juu na meli inaweza kugonga sehemu ile isiyoonekana.
Kwa njia hii jali zinatokea tena na tena na mfano mashuhuri ni ajali ya meli Titanic iliyozama chini mwaka 1912 baada ya kugongwa na siwa barafu. Watu zaidi ya 1,500 walikufa baharini.
| Makala hii kuhusu mambo ya sayansi bado ni mbegu. Je, unajua kitu kuhusu Siwa barafu kama historia yake au mahusiano yake na mada nyingine? Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |