Sikonge

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru


Sikonge
Sikonge is located in Tanzania
Sikonge
Sikonge

Mahali pa Sikonge katika Tanzania

Majiranukta: 5°37′23″S 32°45′17″E / 5.62306°S 32.75472°E / -5.62306; 32.75472
Nchi Tanzania
Mkoa Tabora
Wilaya Sikonge
Idadi ya wakazi
 - Wakazi kwa ujumla 21,298
Ramani ya Wilaya ya Sikonge katika Mkoa wa Tabora, Tanzania.

Sikonge ni kata iliyo makao makuu ya wilaya ya Sikonge katika Mkoa wa Tabora nchini Tanzania yenye postikodi namba 45300.

Katika sensa ya mwaka 2022 wakazi wa kata walihesabiwa 21,298 [1]. Wakati wa sensa iliyofanyika mwaka wa 2012, kata ya Sikonge ilikuwa na wakazi wapatao 17,140 waishio humo.[2]

Sikonge kama mji umegawanyika katika sehemu kuu mbili, Misheni na Madukani. Upande wa Misheni ni sehemu walipojenga Wakristo wa Moravian kanisa lao na misheni yao yaani shule, hospitali na chuo cha uuguzi. Shule yao ya sekondari iko upande wa Madukani. Hamna mgawanyiko maalumu wa Wakristo na Waislamu.

Ila Madukani ni sehemu wanapokaa Waarabu wengi na maduka yao na hiyo imepelekea sehemu hiyo iitwe hivyo. Upande huo pia kuna mahakama, benki, kanisa la Wakatoliki na shule ya sekondari Mbirani. Hiyo ni shule ya siku nyingi sana na ilikuwa ikiitwa Middle School, hivyo wasomi wengi kutoka Sikonge utakuta walisoma hapa. Baadaye ilitaifishwa na kuwa shule ya msingi na si miaka mingi sana ilirudishwa kwa Wamoravian na wakaifanya kuwa shule ya sekondari. Serikali ilijenga shule nyingine mpya na shule hiyo ikachukua jina hilohilo na Mbirani, huku sekondari ikiitwa Sikonge Secondary School.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

Kata za Wilaya ya Sikonge - Mkoa wa Tabora - Tanzania

Chabutwa | Igigwa | Ipole | Kiloleli | Kiloli | Kilumbi | Kipanga | Kipili | Kisanga | Kitunda | Misheni | Mkolye | Mole | Mpombwe | Ngoywa | Nyahua | Pangale | Sikonge | Tutuo | Usunga


Makala hii kuhusu maeneo ya Mkoa wa Tabora bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Sikonge kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
Tafadhali usiingize majina ya maafisa au viongozi wa sasa maana wanabadilika mno.