Shirika la Huduma kwa Wanyama Pori ya Kenya
Shirika la Kenya la Wanyama Pori (KWS - Kenya Wildlife Service) lilianzishwa mwaka 1990. Inasimamia uumbaji na viumbe hai wa nchi, ikilinda na kuhifadhi flora na fauna [0]
KWS inasimamia mbuga za wanyama za Kitaifa na za Hifadhi nchini Kenya. Fedha zinazokusanywa kama ada ya kiingilio katika mbuga hutumika kusaidia uhifadhi wa mimea na wanyama ndani ya hifadhi au mbuga.
Yaliyomo |
Mbuga za Kitaifa na za Hifadhi [hariri]
Kenya ina mbuga 35 teule za kitaifa na za hifadhi:
- Mbuga ya Kitaifa ya Aberdare
- Mbuga ya kitaifa ya Amboseli
- Mbuga ya Kitaifa ya Arabuko Sokoke
- Hifadhi ya Kitaifa ya Arawale
- Hifadhi ya Kitaifa ya Bisanadi
- Hifadhi ya Kitaifa ya Boni
- Mbuga ya Kitaifa ya Central Island
- Mbuga ya Kitaifa ya Milima ya Chyulu
- Mbuga ya Kitaifa ya Hell's Gate
- Hifadhi ya Msitu wa Kakamega
- Mbuga ya Majini ya Kisite-Mpunguti
- Hifadhi ya Paa ya Kisumu
- Mbuga ya Kitaifa ya Kora
- Mbuga ya Kitaifa ya Ziwa Nakuru
- Hifadhi ya Kitaifa ya Losai
- Mbuga ya Kitaifa ya Majini ya Malindi
- Mbuga ya Kitaifa ya Malka Mari
- Mbuga ya Kitaifa ya Marsabit
- Mbuga ya Kitaifa ya Meru
- Mbuga ya Majini ya Mombasa
- Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Elgon
- Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Kenya
- Mbuga ya Kitaifa ya Mlima Longonot
- Hifadhi ya Kitaifa ya Mwea
- Mbuga ya Kitaifa ya Nairobi
- Hifadhi ya Kitaifa ya Ndere Island
- Mbuga ya Kitaifa ya Ol Donyo Sabuk
- Mbuga ya Kitaifa ya Ruma
- Hifadhi ya kitaifa ya Saiwa Swamp
- Hifadhi ya Kitaifa ya Samburu
- Hifadhi ya Kitaifa ya Shaba
- Hifadhi ya Kitaifa ya Milima ya Shimba
- Mbuga ya Kitaifa ya Sibiloi
- Hifadhi ya Nyani ya Mto Tana
- Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Mashariki
- Mbuga ya Kitaifa ya Tsavo Magharibi
- Mbuga ya Majini ya Watamu
Mipango ya Uhifadhi [hariri]
KWS inaendesha mipango maalum kusaidia viumbe na makazi ya Kenya ambayo yako kwenye hatari hasa. Wana mipango ya uhifadhi wa sehemu za chemichemi na misitu,na miradi maalum ya tembo na kifaru kusaidia kuwaokoa kutoka kwa wawindaji. Hirola, ambayo iko katika hatari ya kupotea, pia inafuatiliwa.
Ndani ya KWS kuna huduma kadhaa, kila mmoja ikiwajibika kwa eneo tofauti ya kazi:
Huduma ya Wanyama Pori ya Jamii [hariri]
Hili tawi la KWS hufanya kazi nje ya hifadhi za taifa. Wao badala hufanya kazi katika maeneo kama vile kanda za wanyamapori, na kufundisha jamii wanaoishi huko kuhamasisha uhifadhi na kuchunga rasilimali zao.
Huduma za Usalama [hariri]
Kazi ya huduma hii ni kuondoa uwindaji katika hifadhi za kitaifa, na kukomesha biashara haramu.
Huduma za Matibabu ya Wanyama [hariri]
Huduma hii huhakikisha kuwa afya ya kuzaliana ya wakazi wa aina inazingatiwa kote nchini.
Mafunzo [hariri]
KWS ina kituo cha mafunzo mjini Naivasha. Watumishi wa KWS hufundishwa hapa, na pia mafunzo kwa wanafunzi wa nje wa ikolojia na utalii.
Elimu [hariri]
KWS inendesha vituo kadhaa vya elimu:
- Nairobi Safari Walk
- Kituo cha Elimu cha Nairobi
- Kituo cha Elimu cha Ziwa Nakuru
- Kituo cha Elimu cha Tsavo Mashariki
- Kituo cha Elimu cha Tsavo Magharibi
Hizi ziko ndani ya Hifadhi za Taifa, na uendesha mipango ya kuhamasisha watu kuhudumia na kulinda mazingira yao. NiImelengwa kwa wananchi, hasa makundi ya shule, lakini ni wazi kwa mtu yeyote.