Tezi ya jahazi ya kihistoria
Tezi (au: shetri) ni sehemu ya nyuma ya meli. Hapa kuna usukani wa chombo unaoelekeza meli pale inapotakiwa kuelekea. Ni pia mahali pa rafadha inayosukuma chombo mbele.
Kwa meli kubwa za uvuwi mara nyingi nyavu ya samaki huteremshwa tezini.