Shakwe-mporaji
| Shakwe-mporaji | ||||||||||||||||
|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|---|
| Uainishaji wa kisayansi | ||||||||||||||||
|
Shakwe-waporaji ni ndege wa jenasi Stercorarius, jenasi pekee katika familia Stercorariidae. Pengine huitwa skua pia. Hawa ni ndege wakubwa kadiri ambao wana mnasaba na shakwe. Wana rangi ya kahawa au kijivu; spishi ndogo zina madoa meupe bawani na mileli miwili ya kati ya mikia yao ni mirefu. Wana mdomo mwenye nguvu na ncha kwa umbo la kulabu. Wanaweza kuogelea na kuna ngozi kati ya vidole vya miguu yao.
Ndege hawa wanaweza kupuruka sana na hufukuzia shakwe na ndege wengine wa bahari ili kupora mateka yao (kleptoparasitism). Nyakati nyingine hukamata samaki au hula mizoga na matumbo. Spishi kubwa zinaweza kuua na kula ndege wengine hata mpaka ukubwa wa Shakwe Mgongo-mweusi Mkubwa. Wakati wa majira ya kuzaa hula panya wa tundra (lemming) na mayai na makinda ya ndege wengine. Hutaga mayai yao chini kwa maeneo ya Akitiki.
[hariri] Spishi za Afrika
- Stercorarius longicaudus, Shakwe-mporaji Mkia-mrefu (Long-tailed Skua or Long-tailed Jaeger)
- Stercorarius parasiticus, Shakwe-mporaji wa Akitiki (Arctic Skua or Parasitic Jaeger)
- Stercorarius pomarinus, Shakwe-mporaji Pomarina (Pomarine Skua or Pomarine Jaeger)
- Stercorarius skua, Shakwe-mporaji Mkubwa (Great Skua)
[hariri] Spishi za mabara mengine
- Stercorarius antarctica (Brown Skua)
- Stercorarius chilensis (Chilean Skua)
- Stercorarius maccormicki (South Polar Skua)