Selemani Ndikumana

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Selemani Ndikumana
Maelezo binafsi
Jina kamili Sulemani Yamin Ndikumana
Tarehe ya kuzaliwa 18 Machi 1987 (1987-03-18) (umri 37)
Mahala pa kuzaliwa    Bujumbura, Burundi
Nafasi anayochezea Mshambuliaji
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Lierse S.K.
Namba 18
Klabu za vijana
Inter Star
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2008 Lierse S.K.
Timu ya taifa
2006 Burundi

* Magoli alioshinda

Sulemani Yamin Ndikumana (amezaliwa katika mji wa Bujumbura 18 Machi 1987} ni mchezaji wa mpira wa miguu anaeichezea klabu ya Lierse S.K. katika Ligi ya pili ya Ubelgiji na pia ni mchezaji katika Timu ya Taifa ya Burundi.

Kutoka Norwei nakuelekea Ubelgiji[hariri | hariri chanzo]

Bwana Selemani alijiunga na klabu hiyo ya Lierse S.K. ya Ubelgiji kutoka kwenye klabu ya Molde FK ya Norwei mwaka 2008 mwezi Desemba baada ya klabu hiyo kuweka mkatabu bure na mchezaji huyo baada ya mkataba wa timu yake ya kabla ya Norwei kuisha,klabu hiyo ya Ubelgiji inategemea kuweza kogombea tiketi ya kujiunga katika ligi kuu ya Ubelgiji kwa msaa wa mchezaji huyo mzuri.

Kucheza kwake Ulaya[hariri | hariri chanzo]

Ndikumana Aliacha kuchezea klabu ya Inter Star klabu mashuhuri huko Burundi na alionekana mchezaji mzuri ndio klabu mashuhuri huko Tanzania ikatoa pesa nzuri ili aweze kuchezea klabu hiyo ambayo aliichezea kwa muda mrefu kidogo, baadae klabu ya Molde FK ya Norwei ikaomba kumchukua na alicheza baadhi ya mechi huko Norwei katika klabu hiyo, ila kijana mwenyewe alipiga kelele zaidi kutokana na baridi kali inayopatikana huko Norwei ndio akapata fursa yakujiunga na klabu ya Lierse S.K. huko ambayo ilimuomba nakutegemea anaweza toa mchango mkubwa katika kusaida kupatikina kwa magoli kwa wingi na alinunuliwa mwezi Desemba tar 8.

Jina lake Mashuhuri Burundi[hariri | hariri chanzo]

Jina lake mashuhuri huko Burundi ni Sele Drogba kutokana na uchezaji wake unaofanana na Drogba mwenyewe na katika wachezaji anaopenda duniani pia Drogba akiwemo.

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Selemani Ndikumana kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.