Sayyid

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta

Sayyid (سيد) ni cheo cha heshima cha Kiarabu kinachomaanisha hasa ukoo wa kiume wa Mtume Mohammad.

Yaliyomo

[hariri] Maana ya Kiarabu

Kimsingi "sayyid" yamaanisha "Bwana" ni namna ya kumtaja mtu kwa heshima. Hutumiwa hivyo katika nchi nyingi za Waarabu. Katika lahaja ya Moroko yafupishwa kuwa "sidi" (kutoka sayyidi - Bwana wangu).

[hariri] Maana ya Kiislamu

Hata nje ya Waarabu neno latumiwa kati ya Waislamu kama cheo cha heshima kwa ukoo wa Mtume Muhammad. Mara nyingi lataja wote wanaohusiana na Husain na Hasan wajukuu wa Mtume kupitia binti yake Fatima na Ali ibn Abi Talib.

Mara nyingi ni ukoo wa Husain tu wanaoitwa "sayyid" ilhali ukoo wa Husain wamepewa cheo cha "sharif". Lakini siku hizi "sayyid" hutumiwa pia kwa wote.

Mabinti wa sayyid wa kiume huitwa "sayyida" isipokuwa watoto wa sayyida na baba asiye sayyid hawapokeo cheo hiki.

Kati ya Dawoodi Bohra cheo "syyedina" hutumiwa kwa kiongozi wao mkuu kwa maana ya kimsingi ya Kiarabu "Bwana wetu" hata kama yeye hatoki katika ujoo wa Fatima.

[hariri] Masayyid wa uwongo

Katika historia watu wengi walijipatia cheo hiki kwa sababu ya heshima na pia faida za kiuchumi kwa sababu masayyid walisamehewa kodi mbalimbali katika milki ya Osmani. Hivyo Waosmani waliunda ofisi ya kusimamia Masayyid na kukinga cheo hiki dhidi ya "muhtasayyid" yaani masayyid wa uwongo.


[hariri] Tovuti ya Nje

Harun Yahya kuhusu Sayyid

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine