Saidi Ntibazonkiza

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Saidi
Saidi
Maelezo binafsi
Jina kamili Saidi Ntibazonkiza
Tarehe ya kuzaliwa 1 Mei 1987 (1987-05-01) (umri 36)
Mahala pa kuzaliwa    Bujumbura, Burundi
Nafasi anayochezea Mshambuliaji
Maelezo ya klabu
Klabu ya sasa Young Africans S.C
Namba 10
Klabu za ukubwani
Miaka Klabu
2003-2005
2006-2010
2010-
Vital'O FC
NEC Nijmegen
KS Cracovia
Timu ya taifa
2004- Burundi

* Magoli alioshinda

Saidi Ntibazonkiza (amezaliwa mjini Bujumbura 1 Mei 1987) ni mchezaji wa mpira wa miguu wa kulipwa kutoka Burundi anayechezea klabu ya Yanga Sc ya Tanzania na timu ya taifa ya Burundi.

Kucheza mpira katika ujana wake[hariri | hariri chanzo]

Katika ujana wake alichezea klabu ya Vital'o bingwa wa Burundi. Alichezea timu ya taifa ya umri wa vijana na pia alicheza mechi 7 za timu kuu ya taifa.

Kwenda kwake Uholanzi[hariri | hariri chanzo]

Alikuja Uholanzi mwaka 2005 kwa njia ya kuomba kimbilio la hifadhi ya kisiasa. Klabu ya NEC ilimchunguza na kuona kuwa ni mchezaji ambaye atafaa katika mustakabali kwa hiyo ikamchukua. Kutokana na umri wake mdogo klabu ikamweka katika kikosi cha NEC ya vijana ili kufanya mazoezi na vijana. Kocha wa timu kuu ya NEC, Mario Been, baada ya kuona mchezaji huyo ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo akaona amweke katika timu kuu inayoshiriki katika Ligi Kuu ya Uholanzi. Basi, kijana huyo amecheza mechi nyingi katika Ligi kuu hiyo pakiwemo mechi dhidi ya Ajax Amsterdam na Feyenoord Rotterdam na timu nyingine mashuhuri na alionekana katika mechi hizo kuwa ni mchezaji mzuri.

Kuweka mkataba na NEC[hariri | hariri chanzo]

Mchezaji huyo aliweka mkataba na klabu hiyo, mkataba utakwisha mwaka 2009.

Katika mechi yake ya kwanza aliyoicheza katika kombe la UEFA Cup dhidi ya FC Dinamo Bucuresti alionekana mchezaji mzuri kabisa na alipata zawadi ya mchezaji bora katika mechi hiyo, na kwa sasa mchezaji huyo anacheza dakika zote bila kugombolewa na amekua kiungo muhimu zaidi katika klabu yake kwa sasa, zaidi ya mechi hiyo na picha zakuonyesha kua alipata zawadi hiyo bofya hapa: [1][dead link]

Januari mwaka 2009 aliweka mkataba wakuongeza myaka, ongeza yake hiyo itamfanya abaki kwenye klabu hiyo hadi mwaka 2012 [1]

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu mchezaji mpira fulani bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu Saidi Ntibazonkiza kama wasifu wake, habari za maisha au kazi yake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.
  1. http://www.uefa.com/competitions/uefacup/news/kind=1/newsid=790453.html