Safu ya Ruwenzori
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
(Elekezwa kutoka Ruwenzori)
Safu ya Rwenzori kusini ya Fort Portal (Uganda)
Safu ya Ruwenzori (pia: Rwenzori) ni eneo la milima katika Afrika ya Kati kwenye mpaka wa Uganda na JK Kongo. Mlima wa juu ni Pic Marguerite (Mont Stanley) mwenye kimo cha mita 5109 juu ya UB.
Baada ya Kilimanjaro na mlima Kenya ni mlima mkubwa wa tatu katika Afrika. Pamoja na hii miwili ni milima ya pekee kwenye bara la Afrika penye barafuto za kudumu.
Huaminiwa ya kwamba Rwenzori ni sawa na "Milima ya Mwezi" inayotajwa katika taarifa za Ptolemaio zamani za Misri ya Kale.
| Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika bado ni mbegu. Je unajua kitu kuhusu Safu ya Ruwenzori kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni? Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa? Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari. |