Ruth Bosibori
Ruth Bosibori Nyangau (pia huandikwa kama Ruth Bisibori, alizaliwa 2 Januari 1988 huko Bosiango) ni mwanariadha Mkenya anayekimbia katika mashindano ya umbali wa kati na ni mtaalamu katika shindano la steeplechase mita 3,000.
Mwezi Julai 2007 alikuwa mshindi wa kwanza wa mashindano ya All-Africa Games, kwani ilishindaniwa mara ya kwanza mwaka huo. Mwezi Agosti mwaka uo huo alimaliza wa nne katika Mashindano ya dunia katika rekodi ya dunia ya wanariadha wachanga yadakika 9:25.25. Rekodi ya awali ilikuwa 9:30.70 ilikuwa imewekwa na Melissa Rollison. [1]. Alimaliza wa tatu katika mashindano ya Mabingwa wa Afrika mwaka 2008.
Bosibori alizaliwa katika kijiji cha Bosiango kilicho karibu na Kisii [2] Alianza kukimbia mwaka 2003 alipokuwa katika chuo cha upili cha Kebirichi. Aliajiriwa na Polisi wa Kenya baada ya kushinda michuano ya mkoa mwaka 2007 [3] Amezoea kukimbia mguu tupu.[4]
Alishinda tuzo la Mwanariadha wa kike ambaye ana ahadi zaidi mwaka 2007 katika sherehe za Kenya Sports Personality of the Year[5] Kocha wake ni Dan Muchoki [6]
Mafanikio [hariri]
| mwaka | Mchuano | Ukumbi | Tokeo | Ziada |
|---|---|---|---|---|
| 2007 | All-Africa Games | Alger, Algeria | 1 | 3000 m steeple |
| World Championships | Osaka, Japan | 4 | 3000 m steeple | |
| 2008 | African Championships | Addis Ababa, Ethiopia | 3 | 3000 m steeple |
| Michezo ya Olimpiki | Beijing, Uchina | 6 | 3000 m steeple | |
| World Athletics Final | Stuttgart, Ujerumani | 3 | 3000 m steeple | |
| 2009 | World Championships | Berlin, Ujerumani | 7 | 3000 m steeple |
| World Athletics Final | Thessaloniki, Grekland | 1 | 3000 m s'chase |
Marejeo [hariri]
- IAAF wasifu wa Ruth Bosibori
- ↑ IAAF top orodha - 3000 mita Steeplechase Junior
- ↑ [2] ^ Daily Nation, 2 Novemba 2007: Rekodi ya Bosibori ya dunia yavunjwa
- ↑ [3] ^ The Standard, 19 Agosti 2007: Mnyenyekevu Bosibiri kuendeleza tamaduni
- ↑ [4] ^ Japan Times, 29 Agosti 2007: Worlds notebook; Day 4
- ↑ Soya Awards - 2007 winners
- ↑ IAAF: 4 Agosti 2007: Focus on Africa - Ruta BOSIBORI
| Makala Kenyan biographical relating to athletics bado ni mbegu. Unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuongezea habari. |