Roza Rymbayeva
Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
| Roza Rymbayeva | |
|---|---|
| Jina la kuzaliwa | Roza Kwanyshevna Rymbayeva |
| Amezaliwa | 28 Oktoba 1957 Jangiz-Tobe, Mkoa wa Semipalatinsky, Kazakistani |
| Aina ya muziki | Pop ya Kikazaki |
| Kazi yake | Mwimbaji, mwigizaji |
| Ala | Sauti |
| Miaka ya kazi | 1976–hadi leo |
| Ame/Wameshirikiana na | Sergey Penkin, Batyrkhan Shukenov, Renat Ibragimov, Vladimir Stupin |
| Tovuti | r-rimbaeva.narod.ru |
Roza Kwanyshevna Rymbayeva (alizaliwa tar. 28 Oktoba 1957) ni mwimbaji wa muziki wa Kikazaki na Kirusi kutoka nchini Kazakistani.
Yaliyomo |
Wasifu[hariri]
Maisha ya awali[hariri]
Roza Rymbayeva alizaliwa mkoani Semipalatinsky mnamo tarehe 28 Oktoba 1957 kwa familia ya wafanyakazi wa reli.
Familia[hariri]
Mume — Taskyn Okapov (1948—1999),
Watoto — Ali (1991) na Madi (2000),
Wapwa wa kike wa mumewe — Manshuk (1975) na Aliya (1979).
Filmografia[hariri]
1976 — filamu ya televisheni «Первая песня» (Wimbo wa kwanza), studio «Kazakhtelefilm».
1982 — mwigizaji mkuu wa filamu ya Kisovyeti-Kicheki «До свидания, Медео» (kwa Kirusi) au «Revue na zakázku» (kwa Kicheki)[1]
2001 — filamu «Роза» (Roza), mwogozaji J. Sabirova
2002 — filamu «Хвост кометы. Роза Рымбаева» (mkia wa kometi. Roza Rymbayeva), mwogozaji A. Burykin (Urusi).