Roll Call

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Roll Call
Jina la gazeti Roll Call
Aina ya gazeti Gazeti la misimu
Lilianzishwa 1955
Nchi Marekani Marekani
Mwanzilishi Sid Yudain
Mhariri Charlie Mitchell
Mmiliki Kundi la The Economist Group
Mchapishaji Peter Cherukuri
Makao Makuu ya kampuni *.50 F Street NW
*.Suite 700
Washington DC 20001
Nakala zinazosambazwa 18,379
Tovuti http://www.rollcall.com

Roll Call ni gazeti linalochapishwa jijini Washington D.C. ,Marekani. Gazeti hili huchapishwa Jumatatu hadi Alhamisi wakati ule Congress ya Marekani ipo katika kikao.Pia, huchapishwa Jumatatu katika wakati wa mapumziko. Gazeti hili huwapa wasomaji wake habari kuhusu bunge na siasa zinazoendelea katika Capitol Hill. Mbali na kuwasilisha habari motomoto, gazeti hili hushirikisha habari za Washington D.C. ,makala ya wachambuzi wa siasa kama Morton M. Kondracke, Stuart Rothenberg na Norman Ornstein, na huwasilisha habari za wakati wa uchaguzi wa Congress kote nchini. RollCall.com, tovuti rasmi ya gazeti hili, huwasilisha habari motomoto na pia hutuma arafa kwa watu katika anwani zao kwenye mtandao.

Kundi la Roll Call, ambalo huchapisha gazeti hili, huendesha Gallery Watch ambayo ni tovuti inayofuatilia wabunge na Congress Now ambayo ni tovuti inayoarifu kuhusu sera na sheria katika Capitol Hill.

Ilianzishwa katika mwaka wa 1955 na Sid Yudain, katibu wa zamani wa Al Morano, mwanachama wa Congress. Alikuwa katibu wa kuhusika na vyombo vya habari . Roll Call ,hivi sasa, ni gazetii shirika la Kundi la The Economist. Kampuni zingine shirika ni The Economist, CFO, European Voice na Capital Advantage.

Katika kila toleo, nakala 11,500 za Roll Call huwasilishwa Congress na nakala 400 huwasilishwa White House bila malipo yoyote. Wito wake ni "Gazeti la Capitol Hill Tangu Mwaka wa 1955."

Mnamo Februari 2008,Roll Call ilitangaza uzinduzi wa Roll Call TV. Ikiungana na Robert Traynham, ilitaka kuanzisha kipindi cha dakika 30 cha Jumapili, kingekuwa kipindi cha mahojiano. Kipindi hicho kingeshirikisha waandishi wa habari wa gazeti la Roll Call na wachambuzi wengine wa siasa.

Wafanyikazi mashuhuri wa zamani na wale wa sasa.[hariri | hariri chanzo]

  • Lauren Whittington
  • Susan Glasser, mhariri wa zamani wa kitaifa, Washington Post
  • Glenn Simpson, mfanyikazi mwandishi, Wall Street Journal
  • Jim VandeHei, mhariri mkuui, The Politico
  • Tim Curran, mhariri wa siasa, Washington Post
  • Ed Henry,waandishi wa habari wa White House , CNN
  • Paul Kane, mwandishi wa habari, Washington Post
  • John Bresnahan, mwandishi mkuu wa Congressl, The Politico
  • Mary Ann Akers, mwandishi, washingtonpost.com
  • Ben Pershing, mwandishi, washingtonpost.com
  • Brody Mullins, mwandishi, Wall Street Journal
  • Susan Davis, mwandishi, Wall Street Journal
  • Chris Cillizza, mwandishi, washingtonpost.com
  • Nina Totenberg, mwandishi wa habari, National Public Radio

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]