Roger Scott

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mtangazaji wa redio Roger Scott
Alizaliwa:23 Oktoba 1943
Alikufa:31 Oktoba 1989(umri wa miaka 46)
Uzalendo: Uingereza
Stesheni alizofanya kazi nazo:
Capital Radio
Radio 1
WPTR

Roger Scott (23 Oktoba 1943 - 31 Oktoba 1989) alikuwa Mwingereza aliyecheshimiwa sana katika sekta ya redio. Alikuwa mchaguzi na mchezaji nyimbo katika stesheni za redio. Alifahamika sana kwa kuwasilisha kipindi cha alasiri katika stesheni ya redio ya London,Capital Radio,tangu mwaka wa 1973 hadi mwaka wa 1988.

Alizaliwa jijini London katika mwaka wa 1943, Roger Scott alikuza upendo wa nyimbo za aina ya rock na roll zilizokuwa zikitungwa katika mwisho wa miaka ya 1950 na mapema miaka ya 1960. Akiwa kijana, alianza kucheza muziki karibu na dirisha ya nyumba yao jijini London na kuangalia hisia za wapita njia kwa muziki alizocheza.

Wasifu wa Mapema[hariri | hariri chanzo]

Baada ya muda mfupi kama mfanyibiashara wa baharini,Scott alipata njia na akaingia nchini Marekani na akajiunga na stesheni ya redio ya WPTR ya Albany,New York katika mwaka wa 1966. Kazi ya Scott,kwa sababu ya lafudhi yake ya Uingereza,ilikuwa kuwa 'rafiki wa Beatles' na hapo ndipo Scott akaanza kujifunza kazi ya kuwa mchezaji wa muziki kama DJ akifanya kazi na Boom Boom Brannigan na watu wengine maarufu wa stesheni hiyo. Miezi minane baadaye,alitoka WPTR kuwasilisha kipindi cha jioni katika stesheni ya Montreal ya 1470 CFOX. Kutoka mwaka wa 1967 hadi mwaka wa 1971 akapendwa katika stesheni hiyo kwa mitindo yake ya uwasilishaji na upendo wake wa dhati wa muziki. Hasa wakati huu alishiriki katika Give Peace A Chance iliyorekodiwa na John Lennon na Yoko Ono walipokuwa katika Hoteli ya Queen Elizabeth jijini Montreal.

Makao makuu ya Capital Radio London.Roger Scott alifanya kazi miaka kumi na mitano na stesheni ya Capital Radio

Akitarajia uzinduzi wa stesheni za kibiashara za redio,Scott alirudi Uingereza katika mwaka wa 1971,lakini akapata maendeleo hayakuwa mbele kama alivyofikiri. Wakati uo huo, yeye alipata nafasi ya kazi katika UBN,stesheni ya kampuni ya United Biscuits, iliyotangaza habari kwa viwanda vya kampuni hiyo katika taifa zima. Ilikuwa wakati huu ,pia, alifanya kazi katika stesheni ya BBC Redio lakini akingoja kazi ya baadaye katika redio ya kibiashara alifanya kazi hiyo chini ya jina "Bob Baker."

Wasifu[hariri | hariri chanzo]

Capital Radio[hariri | hariri chanzo]

Redio za kibiashara ,hatimaye,zilipewa mamlaka katika mwaka wa 1972 na katika mwaka wa 1973 alijiunga na wafanyikazi wa stesheni ya London,Capital Radio. Vipindi vya alasiri vya Scott vikapata umaarufu sana baina ya wakazi wa London, akizalisha vipindi maarufu kama Three O'Clock na Hitline pamoja na wimbo wa Grab a a little piece of heaven ulioimbwa na David Dundas. Katika mwaka wa 1976, kipindi chake cha mara kwa mara cha Ijumaa cha kucheza nyimbo za kitambo kilipata mashabiki wa dhati. Hasa,kwa sababu ya Scott kuchezesha nyimbo zisizojulikana za aina ya rock-a-billy kwa mara ya kwanza.

Scott hakufuata orodha za kawaida za muziki , utafiti wowote wa wasikilizaji ama mbinu zozote za stesheni za kibiashara katika miaka ya 1980.Alitumia mbinu zake.

Radio 1[hariri | hariri chanzo]

Nembo ya BBC Radio 1

Katika mwezi wa Juni 1988,baada ya miaka kumi na mitano katika Capital, alihamia stesheni isiyo ya kibiashara ya BBC Radio 1. Akiwa huko,alifikia wasikilizaji wa taifa zima kwa mara ya kwanza,akiwasilisha kipindi cha alasiri cha Jumamosi na kipindi cha usiku cha Jumapili. Katika kipindi cha Jumamosi,alihusisha mahojiano na wanamuziki maarufu wengi kama Dion,Jackson Browne,Don Henley na wengine wengi. Vipindi vyake vya Jumapili vimekuwa vya kufurahisha hasa ikishirikisha muziki ya rock na roll ya miaka ya 1950 na muziki ya aina nyingi.

Roger Scott aliaga dunia katika mwaka wa 1989,akiwa umri wa miaka wa 46, baada ya kuugua kansa kwa muda mfupi.

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

marejeo haya yako katika lugha ya Kiingereza

  1. Roger Scott talks about his early career
  2. Roger Scott on CFOX in 1969
  3. Roger Scott talks about the John Lennon "bed in" in Montreal
  4. Elton John on Roger Scott's Capital show, including Elton singing Roger's 'Grab a little piece of heaven' jingle
  5. Roger Scott talks about playlists and market research

Viungo vya nje[hariri | hariri chanzo]