Richard wa Chichester
Richard wa Chichester (1197 - Dover, 3 Aprili 1253) alikuwa askofu wa Uingereza ambaye alipigania adhimisho la ekaristi lifanyike kwa heshima, sakramenti zitolewe bure kwa waamini na makasisi washike vema useja kwa ajili ya ufalme wa mbinguni.
Yaliyomo |
[hariri] Kijana
Ujanani alitakiwa kufanya kazi nzito ili kutegemeza familia yake. Baadaye aliweza kwenda masomoni kwenye chuo kikuu cha Oxford, chini ya Edmund Rich na Grosseteste, halafu Paris na Bologna.
[hariri] Katibu mkuu wa jimbo
Akiwa na umri wa miaka 38 akarudu Oxford, alipochaguliwa mara awe gombera wa chuo kikuu, lakini mwaka 1237 mwalimu wake wa zamani Rich, kisha kuchaguliwa Askofu mkuu wa Canterbury, alimtaka awe katibu mkuu wa jimbo lake; katika kazi hiyo alijitokeza katika jitihada za kurekebisha mwenendo wa mapadri na kupinga uvamizi wa serikali katika mamlaka ya Kanisa.
[hariri] Padri
Aliposhuhudia kifo cha askofu wake huko Soissy Ufaransa mwaka 1240, na kuachiwa kikombe kama urithi, aliamua kuingia upadri akaenda kusomea teolojia miaka miwili kwa Wadominiko wa Orléans.
Baada ya kupadirishwa mwaka 1242 akiwa na miaka 45, akarudi Uingereza na kufanya kazi ya paroko Charing na Deal (mkoa wa Kent), lakini akarejeshwa mapema katika ukatibu mkuu.
[hariri] Askofu
Mwaka 1244 alichaguliwa na maaskofu kuongoza jimbo la Chichester, lakini mfalme Henry II alimtaka Richard Passelewe, hivyo akazuia mali na mapato ya jimbo.
Papa Inosenti IV alipoombwa usuluhisho alimtibithisha na kumweka wakfu mwaka 1245 huko Lyons.
Askofu mpya aliporudi Chichester, alilazimika kuishi kifukara katika nyumba ya paroko wa Tarring (Sussex), akifanya kazi za mikono na kutembelea jimbo lote kwa miguu. Miaka miwili baadaye mfalme Henry III alilazimishwa na Papa kulirudishia jimbo mali zote.
[hariri] Matendo ya upendo
Richard alikuwa mkarimu sana na mpole kwa wakosefu. Alitunga sheria za jimbo, ambazo zinadumu hadi leo, kuhusu masuala mbalimbali. .
[hariri] Kifo na heshima
Akiwa Dover ili kumjengea kanisa hayati mwalimu wake Edmund Rich, aliugua sana akafa tarehe 3 Aprili 1253.
Miaka tisa baadaye, Papa Urbanus IV, alimtangaza kuwa mtakatifu tarehe 22 Januari 1262.