Reykjavík

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Mji wa Reykjavik

Reykjavík (tamka: reykyavik) ni mji mkuu pia mji mkubwa wa Iceland mwenye wakazi 113,387. Ni mjii mkuu wa dunia ulio kaskazini zaidi kushinda miji mikuu ya nchi zote huria.

Jiografia[hariri | hariri chanzo]

Iko kwenye pwani la kusini la Iceland mwabaoni wa hori ya Faxaflói.

Reykjavik inafaidika na kukaa kwenye mahali pa kukutana kwa mabamba ya gandunia ya Ulaya na Amerika ya Kaskazini. Magma ya koti ya dunia iko karibu na uso wa nchi inasababisha maji kwenye ardhi kuwa moto. Maji ya moto haya hutumiwa kwa kupasha moto nyumba za kukalia watu pia bustani za mabandani. Nishati inapatika kwa rahisi kiasi cha kwamba katika mazingira ya barafu kuna hata mavuno ya ndizi kwenye bustani za mabandani zinazopashwa moto kwa maji yale ya chini ya ardhi.

Historia[hariri | hariri chanzo]

Inaaminiwa ya kwamba Reykjavík ilikuwa mahali pa makazi ya kwanza ya watu walioanza kufika kisiwani mnamo mwaka 870. Mwanzilishaji wa makazi alikuwa Mnorway Ingólfur Arnarson. Hadi karne ya 18 hapakuwa na mji bali rundiko la nyumba za wakulima tu.

Mji mwenyewe ulianzishwa hapa mwaka 1786 kama kituo cha biashara ikaendelea kukua.

Leo hii ni mji wa kisasa kabisa na kitovu cha uchumi, utamaduni na siasa wa Isilandi.

Hali ya hewa[hariri | hariri chanzo]

Hali ya hewa Reykjavik

Kutokana na mahali pake karibu na ncha ya kaskazini Reykjavik haioni giza ya usiku kabisa wakati wa miezi Mei - Julai lakini wakati wa Novemba - Januari kuna massa manne tu za mwanga wakati wa machana.

Picha za Reykjavik[hariri | hariri chanzo]

Makala hii kuhusu maeneo ya Ulaya bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Reykjavík kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.