Rasi ya Tumaini Jema

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rasi za Tumaini Jema na Agulhas nchini Afrika Kusini.
Rasi ya Tumaini Jema kutoka Cape Point.

Rasi ya Tumaini Jema (kwa Kiingereza Cape of Good Hope) ni mkono wa nchi unaoingia katika Atlantiki kusini mwa bara la Afrika karibu na mji wa Cape Town (Afrika Kusini). Si mahali pa kusini kabisa mwa Afrika ambapo ni Rasi Agulhas.

Jina limetokana na wapelelezi Wareno waliofika huko mnamo mwaka 1488. Baada ya kutafuta kwa muda mrefu njia ya kufika Uhindi kwa njia ya bahari waliona huko tumaini kwa sababu pwani ilikwisha kuelekea kusini. Mreno wa kwanza aliyeiona alikuwa Bartolomeu Dias.

Makala hii kuhusu maeneo ya Afrika Kusini bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Rasi ya Tumaini Jema kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.