Punjab (Uhindi)

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Moja ya Sehemu ya mji ndani ya jimbo la wa Punjab
Mahali pa Punjab katika Uhindi

Punjab ( Kipunjabi:ਪੰਜਾਬ, Kihindi पंजाब) ni jimbo la Uhindi lililopo katika kaskazini magharibi ya nchi hii. Ni sehemu ya eneo la kihstoria ya Punjab iliyogawiwa kati ya Pakistan na Uhindi na kila upande tena kwa majimbo mbalimbali yenye majina tofauti.

Punjab ya Kihindi ina wakazi milioni 24.3 na eneo lake ni 50,362 km². Mji mkuu ni Chandigarh ambayo ni pia mji mkuu wa jimbo jirani la Haryana kwa hiyo si sehemu ya eneo la jimbo lakini inahesabiwa kama eneo la pekee.

Miji mingine muhimu ni Mohali, Ludhiana, Amritsar, Bathinda, Patiala and Jalandhar.

Imepakana na jimbo la Punjab katika Pakistan, majimbo ya Kihindi Jammu na Kashmir upande wa kaskazini, Himachal Pradesh upande wa kaskazini mashariki, eneo maalumu la Chandigarh upande wa mashariki, Haryana upande wa kusini na Rajasthan upande wa kusini magharibi.


Makala hii kuhusu maeneo ya Uhindi bado ni mbegu.
Je unajua kitu kuhusu Punjab (Uhindi) kama historia yake, biashara, taasisi zilizopo, watu au utamaduni?
Labda unaona habari katika wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.