Prekilampsia

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Prekilampsia
Mwainisho na taarifa za nje
SpecialtyObstetrics Edit this on Wikidata
ICD-10O11., O14.
ICD-9642.4-642.7
DiseasesDB10494
MedlinePlus000898
eMedicinemed/1905 ped/1885
MeSHD011225

Prekilampsia (PE) ni ugonjwa wa ujauzito unaodhihirika kwa shinikizo la juu la damu na kiwango kikubwa cha protini kwenye mkojo.[1] Ugonjwa huu hutokea katika trimesta ya tatu ya ujauzito na huzidi jinsi muda unavyoendelea.[2][3] Katika hali mbaya ya ugonjwa huu, hali zifuatazo zinaweza kuwepo: umeng’enyaji wa seli nyekundu za damu, upungufu wa idadi ya chembe za kugandisha damu, kuharibika kwa utendaji wa ini, utendakazi duni wa figo, kuvimba, ugumu wa kupumua kufuatia kuwepo kwa kiowevu kwenye mapafu, au matatizo ya macho.[2][3] PE huongeza hatari ya kuathirika kwa mama na mtoto.[3] Hali hii isipotibiwa inaweza kusababisha mtukutiko, ambapo hujulikana kama eklampsia.[2]

Kisababishi na utambuzi[hariri | hariri chanzo]

Vipengele vya hatari vya PE hujumuisha: unene, hipatensheni iliyotokea awali , uzee, na kisukari tamu.[2][4] Hali hii pia hutokea mara nyingi zaidi katika mimba ya kwanza ya mwanamke na ikiwa anabeba pacha.[2] Utaratibu wa kimsingi huhusisha utaratibu usio wa kawaida wa kuundika kwa mishipa ya damu kwenye plasenta kando na vipengele vingine.[2] Visa vingi hutambuliwa kabla ya kuzaa. Mara nadra, prekilampsia inaweza kuanza kipindi cha baada ya kuzaa.[3] Ingawa kihistoria shinikizo la juu la damu na uwepo wa protini kwenye damu ni vipengele vya kuthibitisha utambuzi wa ugonjwa huu, fasili zingine pia zinajumuisha vilivyohitajika hipatensheni na ukosefu wa utendakazi wowote wa viungo.[3][5] Shinikizo la damu hufasiliwa kama la juu likizidi mmHg 140  la sistoli au mmHg 90  la diastoli nyakati mbili tofauti, vya tofauti ya zaidi ya saa nne katika wanawake baada ya wiki ishirini za ujauzito.[3] PE huchunguzwa mara kwa mara wakati wa utunzaji wa kabla ya kuzaa.[6]

Kinga na matibabu[hariri | hariri chanzo]

Mapendekezo ya kinga ni pamoja na: aspirin kwa watu walio katika hatari kubwa, nyongeza ya kalisi katika maeneo yenye upungufu wake na matibabu dhidi ya hipatensheni ya awali kwa dawa.[4][7] Kwa watu walio na PE, kutolewa kwa fetasi na plasenta ni njia bora ya matibabu.[4] Kupendekezwa kwa kutolewa kwa fetasi na plasenta hutegemea kiwango cha PE na ukubwa wa ujauzito.[4] Dawa za shinikizo la damu, kama vile labetalol na methyldopa, zinaweza kutumika kuboresha hali ya mama kabla ya kuzaa.[8] Salfeti ya magnesiamu inaweza kutumika kuzuia eklampsia kwa watu walio na hali mbaya ya ugonjwa huu.[4] Kupumzika na kutumia chumvi ni mbinu ambazo hazijabainika kusaidia kukinga wala kutibu ugonjwa huu.[3][4]

Prekilampsia huathiri kati ya asilimia 2–8 ya wanawake wajawazito kote duniani.[4] Magonjwa ya shinikizo la juu la damu wakati wa ujauzito ni mojawapo ya visababishi vikuu vya vifo vinavyotokana na ujauzito.[8] Magonjwa haya yalisababisha vifo 29,000 mwaka wa 2013 – vilivyopungua kutoka vifo 37,000 mwaka wa 1990.[9] Prekilampsia kawaida hutokea baada ya wiki 32; hata hivyo, ikitokea mapema, madhara mabaya zaidi hutarajiwa.[8] Wanawake ambao walipata PE awali wako katika hatari zaidi ya magonjwa ya moyo baadaye maishani.[6] Neno eklampsia linatokana na neno la Kigiriki linalomaanisha radi.[10] Maelezo ya kwanza yanayofahamika yalitolewa na Hippocrates katika karne ya 5 BCE.[10]

Marejeo[hariri | hariri chanzo]

  1. Eiland, Elosha; Nzerue, Chike; Faulkner, Marquetta (2012). "Preeclampsia 2012". Journal of Pregnancy 2012: 1–7. doi:10.1155/2012/586578. 
  2. 2.0 2.1 2.2 2.3 2.4 2.5 Al-Jameil, N; Aziz Khan, F; Fareed Khan, M; Tabassum, H (February 2014). "A brief overview of preeclampsia.". Journal of clinical medicine research 6 (1): 1–7. PMID 24400024.  Check date values in: |date= (help)
  3. 3.0 3.1 3.2 3.3 3.4 3.5 3.6 "Hypertension in pregnancy. Report of the American College of Obstetricians and Gynecologists’ Task Force on Hypertension in Pregnancy.". ObstetGynecol. 122 (5): 1122–31. Nov 2013. PMID 24150027. doi:10.1097/01.AOG.0000437382.03963.88. Ilihifadhi kwenye nyaraka kutoka chanzo mnamo 2016-01-06. Iliwekwa mnamo 2016-03-11. 
  4. 4.0 4.1 4.2 4.3 4.4 4.5 4.6 WHO recommendations for prevention and treatment of pre-eclampsia and eclampsia. 2011. ISBN 978-92-4-154833-5. 
  5. Lambert, G; Brichant, JF; Hartstein, G; Bonhomme, V; Dewandre, PY (2014). "Preeclampsia: an update.". Actaanaesthesiologica Belgica 65 (4): 137–49. PMID 25622379. 
  6. 6.0 6.1 Steegers, Eric AP; von Dadelszen, Peter; Duvekot, Johannes J; Pijnenborg, Robert (August 2010). "Pre-eclampsia". The Lancet 376 (9741): 631–644. PMID 20598363. doi:10.1016/S0140-6736(10)60279-6.  Check date values in: |date= (help)
  7. Henderson, JT; Whitlock, EP; O'Connor, E; Senger, CA; Thompson, JH; Rowland, MG (May 20, 2014). "Low-dose aspirin for prevention of morbidity and mortality from preeclampsia: a systematic evidence review for the U.S. Preventive Services Task Force.". Annals of internal medicine 160 (10): 695–703. PMID 24711050. doi:10.7326/M13-2844.  Check date values in: |date= (help)
  8. 8.0 8.1 8.2 Arulkumaran, N.; Lightstone, L. (December 2013). "Severe pre-eclampsia and hypertensive crises". Best Practice & Research Clinical Obstetrics &Gynaecology 27 (6): 877–884. doi:10.1016/j.bpobgyn.2013.07.003.  Check date values in: |date= (help)
  9. GBD 2013 Mortality and Causes of Death, Collaborators (17 December 2014). "Global, regional, and national age-sex specific all-cause and cause-specific mortality for 240 causes of death, 1990-2013: a systematic analysis for the Global Burden of Disease Study 2013.". Lancet. PMID 25530442. doi:10.1016/S0140-6736(14)61682-2.  Check date values in: |date= (help)
  10. 10.0 10.1 Emile R. Mohler (2006). Advanced Therapy in Hypertension and Vascular Disease. PMPH-USA. ku. 407–408. ISBN 9781550093186.