Precision Air

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Nembo ya Precision Air

Precision Air ni ndege iliyo na makao yake mjini Dar Es Salaam nchini Tanzania. Inahudumia watalii na wafanyibiashara wanaosafiri kwenye viwanja vya ndege 10 nchini Tanzania, pamoja na ndege za kwenda nchi ya Kenya na Uganda. Makao yake makuu ni kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, mjini Dar es Salaam na ikiwa na vituo kwenye viwanja vya ndege vya Kilimanjaro, Arusha na Mwanza.

Yaliyomo

[hariri] Historia

Precision Air ilianzishwa mnamo 1991 na kuanza huduma mnamo 1994. Hapo awali, kampuni hii ilikuwa ya kibinafsi, lakini Kenya Airways ilinunua 49% kwa $ milioni 2, wiki chache tu baada ya South African Airways iliponunua 49% ya Air Tanzania. Asilimia 51 iliyobaki ilikuwa ni wa Michael Ngaleku Shirima.[1] /Kuanza october 2011,Precision air iliamua kuanza kuuza hisa zake katika soko la hisa la Dar es salaam na hivyo umilika wa Ndugu Michael Shirima na Kenya Airways utapungua mpaka Asilimia 33 kila moja.Kuanzia mwezi oktoba 2011 shirika la precisionair limeanza kuuza hisa zake kwa umma wa watanzania.Michael Shirima alitoa nusu ya hisa zake na Kenya airways wakatoa nusu ya hisa zao.kwa hivyo theluthi moja ya hisa hizo itamilikiwa na umma wa watanzania.bei ya hisa moja inauzwa kwa tshs 475 kwa hisa moja.

[hariri] Miji inayosafiria

Precision Air nchini Kenya.

Precision Air inasafiri hadi miji ya Dar es Salaam, Arusha, Kigoma, Kilimanjaro, Musoma, Mwanza, Shinyanga, Tabora, Zanzibar, Mombasa, Nairobi na Entebbe.[Johanesburg][Hahaya][Bukoba] Mkakati wa kwenda katika maeneo mengine bado upo

[hariri] Ndege zake

Hadi Agosti 26, 2009, Precision Air ina ndege zifuatazo:

  • Ndege 4aina ya ATR42-400'
  • Ndege 5 aina ya ATR 72-500
  • Ndege 2 aina ya Boeing 737-300

[hariri] Zilizowekwa oda

  • Ndege 2 aina ya ATR 42-500
  • Ndege 1 aina ya ATR 72-500
  • Majina ya ndege hizo ni 5HPAA,5HPAG,5HPWE na 5HPWF ambazo ni ATR42
  • Nyingine ni 5HPWA,5HPWB,5HPWC,5HPWD na 5HPWG ambazo ni ATR72
  • Vile vile wana BOEING 737-300 mbili ambazo ni 5HPAZ na 5HPMS

[hariri] Marejeo

[hariri] Viungo vya nje

Vifaa binafsi
Maeneo ya wiki

Vibadala
Vitendo
Urambazaji
Vifaa
Lugha zingine