Paulo wa Tebe

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Rukia: urambazaji, tafuta
Picha ya Kikopti ya Paulo wa Tebe.
Mt. Antoni abati na Mt. Paulo Mkaapweke walivyochorwa na Diego Velázquez, 1635 hivi - Museo del Prado, Madrid (Hispania).
Mt. Antoni abati na Mt. Paulo Mkaapweke.

Paulo wa Tebe (230 hivi - Jangwa la Tebais, 335 hivi) anajulikana kama mkaapweke wa kwanza.

Anaheshimiwa tangu zamani sana kama mtakatifu. Sikukuu yake inaadhimishwa kila tarehe 15 Januari.

Chanzo cha habari kuhusu maisha yake ni kitabu cha Jeromu, Vita Sanctii Pauli primi eremitae, kilichoandikwa katika nusu ya pili ya karne IV.

Wakati wa dhuluma ya Kaisari Decius, Paulo, kijana msomi na tajiri wa Misri, alilazimika kukimbia mji wake na kwenda jangwani kisha kushtakiwa na jamaa zake (waliotamani kujipatia mali yake) kuwa ni Mkristo.

Baada ya dhuluma hiyo kali kwisha mapema, Paulo hakurudi nyuma, bali aliendelea kuishi upwekeni hadi kifo chake.

Alipokaribia kufa alitembelewa na Antoni Abati, akamuomba amzike amefunikwa joho alilopewa na Atanasi wa Aleksandria.

Vyanzo kwa Kiswahili[hariri | hariri chanzo]

  • Misemo ya Mababa wa Jangwani (Apophthegmata Patrum) – tafsiri ya W. Ngowi, O.F.M.Cap. – ed. Salvatorianum – Morogoro 2000ISBN 0-264-66350-0